Thursday, October 22, 2020

RONALDO MSHINDI WA TUZO YA BALLON D’OR

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

MADRID, Hispania

CRISTIANO Ronaldo atanyakua tuzo ya nne ya Ballon d’Or kwa mujibu wa taarifa zilizovujishwa na mtandao wa Mundo Deportivo.

Baada ya kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa akiwa Real Madrid na lile la Euro 2016 na kikosi cha Ureno, mshambuliaji huyo amepewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo hiyo.

Mtandao wa Mundo Deportivo umesema utafanya mahojiano na mshindi leo kwa ajili ya mahojiano hayo kurushwa Jumatatu ya wiki ijayo kwenye sherehe ya kumtangaza mshindi wa tuzo hiyo.

Hivyo Ronaldo pamoja na hasimu wake Lionel Messi na Antoine Griezmann watajulishwa mapema matokeo hayo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 alinyakua tuzo hiyo kwa mara ya kwanza akiwa Manchester United mwaka 2008, kabla ya Messi kubeba tuzo hiyo mwaka uliofuata.

Kuanzia mwaka 2010-15, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lilichukua tuzo hizo na kubadilisha mfumo wa kupiga kura.

Messi aliendelea kunyakua tuzo hiyo mara mara zingine tatu na kuwa mchezaji wa kwanza kunyakua tuzo hiyo mara nne mfululizo.

Lakini Ronaldo alibeba tena tuzo hiyo ya Ballon d’Or mwaka 2013, kabla ya kufanua hivyo tena mwaka uliofuata na kuwa mchezaji wa tano kunyakua tuzo hiyo mara tatu.

Mafanikio ya Barcelona ya kuanya mataji matatu msimu wa 2015, ilimfanya Messi kuweka rekodi ya kunyakua tuzo hiyo mara tano.

Wawili hao wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuendelea kupigania tuzo hiyo mwakani, ingawa wachezaji kama Griezmann, Gareth Bale, Neymar, Luis Suarez na hata Eden Hazard wanaweza wakawapa upinzani.

Kaka ndio mchezaji mwingine wa mwisho kunyakua tuzo hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -