MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amekiri kwamba anaweza kucheza pembeni ya Wayne Rooney kwa mara nyingine, umeandika mtandao wa MirrorFootball. Mshindi huyo mara tatu Ballon d’Or aliachana na Rooney na Manchester United na kutimkia Real Madrid mwaka 2009, lakini bado anatamani kucheza pamoja na mshambuliaji huyo wa England.