Sunday, October 25, 2020

Rooney ashauriwa kuondoka Man Utd

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

MANCHESTER, England

MHARIRI wa Michezo wa mtandao wa Sun, Charlie Wyett, amemshauri mshambuliaji wa Manchester United, Wyane Rooney, kuondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na timu ambayo atacheza kama kiungo wa kati.

Rooney alizomewa katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia kati ya England na Malta, ambapo Three Lions walishinda mabao 2-0 katika Uwanja wa Wembley, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mchezo huo, Rooney alicheza pembeni ya Jordan Henderson, lakini kocha wa muda wa England, Gareth Southgate, alimtetea mchezaji huyo baada ya mechi, akisema si sawa kumkosoa nyota huyo.

Rooney amewekwa benchi kwenye mechi takribani tatu zilizopita za Man United na mhariri huyo wa Sun, Wyett amesema mchezaji huyo anapaswa kufikiria kuondoka Old Trafford na kuangalia klabu nyingine ambayo itampa nafasi ya kucheza kiungo wa katikati na si pembeni.

“Itakuwa ngumu, lakini Rooney anapaswa kuondoka majira ya kiangazi yajayo na kwenda kucheza sehemu nyingine mwakani, ambapo kila wiki atacheza kama kiungo wa katikati na si pembeni,” alisema Wyett.

“Najua United hawatakuwa tayari kumuachia aondoke na Rooney mwenyewe hatakuwa tayari kuondoka Manchester United. Lakini kama anataka acheze England, itabidi atafute timu ambayo itampa nafasi ya kucheza katikati lakini si kupangwa pembeni kama winga.

“Tatizo ni kwamba kocha wake, Jose Mourinho, hana kabisa mpango wa kumchezesha katikati, hivyo Rooney hataweza kupata nafasi ya kucheza England kama hana nafasi ya kucheza pale katikati kwenye klabu.”

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -