Wednesday, October 21, 2020

ROONEY, JICHO LAKO LISITAZAME SURA ZAO BALI MIOYO YAO

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HALID MTUMBUKA

KUNA ukweli mmoja tu kwa sasa juu ya Wayne Rooney na Manchester United. Ukweli wenyewe ni kwamba, ameifikia ile rekodi aliyokuwa akiiwazia ingawa mwenyewe hakuwahi kuweka wazi juu ya kuwa na hamu ya jambo hilo, rekodi ya kumfikia Sir Bobby Charlton ya kuwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya Manchester United.

Bao lake dhidi ya Reading limemfanya kufikisha idadi ya mabao 249 ambayo ni idadi sawa na Bobby.

Mwenyewe alikuwa jukwaa kuu siku ile akiiangalia miguu ya Rooney kwenye mfumo wa Jose Mourinho, sina shaka alifurahia na alihuzunika kwa wakati huo huo.

Alifurahia kwa kuwa Rooney ndiye aliyeivunja rekodi hiyo lakini alihuzunika kwa kuwa alitamani kila inapotajwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya Old Trafford, basi litajwe jina lake, tunapaswa kuamini hivyo kwa kuwa hakuna asiyependa kutajwa kwenye mafanikio.

Ni binadamu mmoja tu aliyekataa kutajwa kwa mafanikio, naye si mwingine bali ni Fidel Castro, huyu jamaa alizaliwa na moyo wa kipekee sana, moyo alioukosa Balack Obama, kwani si ulimsikia akitaja mafanikio yake katika hotuba yake ya mwisho? Binadamu wengi tumezaliwa hivyo nasi dhambi kuelezea mafanikio yako.

Lakini pamoja na kuifikia rekodi ya Bobby Charlton, ni shabiki gani wa Manchester United atakayeifurahia rekodi hiyo na kuja mbele ya ulimwengu kujinadi kwa furaha au kujivunia kuwa na Wayne Rooney kwenye kikosi cha United chini ya Jose Mourinho kama ilivyo kuwa chini ya Sir Alex Farguson? Ni nani huyo? Anatokea pande ipi ya dunia?

Sifikirii kama yupo hapa ulimwenguni kwa wakati huu, hayupo. Huo ndio ukweli uliopo kwa sasa, achana na mashabiki wa United waliosambaa dunia nzima ikiwamo Tanzania, siku ile nilijaribu kusoma maoni ya mashabiki wa United wanaolipa viingilio kila United inaposhuka dimbani, waliolipia tiketi za msimu mzima hakuna aliyeonesha kwamba Rooney kuifikia rekodi ya Bobby Charlton, kwake lilikuwa jambo kubwa lililomgusa moyo wake na pengine kutamani dunia ifahamu hilo kwa uzito mkubwa.

Wengi walimpongeza tu Rooney kwa kuifikia rekodi hiyo na wapo waliomkosoa. Lakini ukweli haupingiki kwamba Rooney ndiye mfalme mpya ajae kwenye kikosi cha Manchester United, ukweli haupingiki na upo mmoja tu duniani.

Kwanini mashabiki wa United hawana imani sana juu yake? Sababu ni moja tu, Rooney hakimbii tena na mipira kwenye robo tatu ya mwisho ya United na kuwafanya walinzi wa timu pinzani kumhofia na kutembea sanjari naye pindi anapokuwa na mpira mguuni. Wengine wanatamani asiwepo kwenye kikosi chao kwa sasa licha ya kuonesha kiwango kizuri aliporejea kutoka majeruhi na kufunga bao moja dhidi ya Reading.

Ukweli ni kwamba, Rooney wa sasa mwenye nywele kichwani mwake chini ya Jose Mourinho, si yule aliyekuwa na kipara chini ya Sir Alex Furguson.

Rooney huyu mwenye miaka 31 ni ngumu mno kumuona akikimbia umbali mrefu na kusumbuana na walinzi kama ilivyokuwa nyakati zile chini ya Sir Alex Furguson. Maisha yapo hivyo na ukweli upo hivyo.

Kwa sasa tutafurahi zaidi akicheza nyuma ya Marcus Rashford kwenye eneo la ushambuliaji kuliko ile nafasi tunayohitaji acheze. Inawezekana mashabiki wa United wanaisubiri kwa hamu siku ambayo miguu yake itafunga bao la 250, ndipo wajivunie zaidi kuwa na Rooney lakini nani anajua?

Nilivyofikiria hilo nikakumbuka kwamba mashabiki wa United wanachokitaka kwa sasa ni mataji kuliko kitu chochote kile hapa ulimwenguni! Watamfurahia Rooney pindi atakapowapa wanachokihitaji kuliko anachokihitaji Rooney mwenyewe. Rooney jicho lako lisiishie tu kutazama sura zao za furaha juu yako kwa sasa, bali litazame ndani ya mioyo yao. Furaha yao mashabiki wako ni kukuona ukikokota mipira kwa faida na ukitembea na mipira kwa faida kuelekea kwenye robo tatu ya mwisho ya eneo la ushambuliaji na kuipatia matokeo Manchester United.

Lakini United inaonekana kuimarika hivi sasa tofauti na wakati kikosi hicho kikianza, sijui kwanini hawapewi  heshima hivi sasa, nawaaangalia kwa jicho la kipekee, si tu kushinda michezo sita mfululizo kwenye Premier League, bali hata namna wanavyocheza na kuanzisha mashambulizi yao.

Antonio Valencia kule pembeni ameituliza akili ya Mourinho na kumfanya asifikirie tena juu ya suala la kuingia sokoni, anakimbia na mpira na kupiga krosi zenye faida kwa timu yake na ni ngumu mno kumuona hatimizi majukumu yake ipasavyo.

Hata Rooney mwenyewe nyuma ya Rashford kwenye idara ya ushambuliaji wanatembea na mipira na kutafuta mianya ya upatikanaji wa mabao, Juan Matta, Ander Herrera wamekuwa na msaada mkubwa kwenye kiungo pamoja na Paul Pogba, United inazidi kuimarika taratibu kinyume na wengi wanavyoifikiria.

Tatizo moja la wapenzi wa mpira wa miguu hususani mashabiki wa Manchester United ni kwamba, hawana macho kama waliyonayo kina Arsene Wenger, Jose Mourinho, Antonio Conte na makocha kadhaa juu ya klabu na wachezaji wao, jicho la mashabiki juu ya Rooney ni tofauti na jicho la Mourinho juu ya Rooney, mashabiki wataiangalia miguu yake kwa namna moja tu wakati Mourinho atamwangalia Rooney kwa namna zaidi ya moja na ni hapo atakapoendelea kumwamini kwa namna atakavyoona inafaa.

Hata mashabiki wa Arsenal humwangalia Olivier Giroud kwa jicho la tofauti na Wenger anavyomwangalia. Rooney jiangalie tofauti na unavyoangaliwa na uwaangalie wanaokuangalia tofauti pia kuanzia juu ya sura zao hadi chini ya vungu za mioyo yao na hapo ndipo utakapogundua unachohitaji kukifanya kwa wakati huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -