Tuesday, January 19, 2021

RUBBY AIBUKIA UZALENDO KWANZA, AAHIDI KUFANYA MAKUBWA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA KYALAA SEHEYE

UZALENDO Kwanza ni umoja wa watu maarufu katika fani mbalimbali ambao wamepania kutangaza uzalendo nchi nzima, huku wakishiriki katika shughuli mbalimbali za jamii na kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ili kuweka maana ya kauli mbiu yao.

Umoja huu, ambao unaunganisha wasanii wa filamu, muziki, wachezaji mpira na Watanzania wa kawaida na kwa yeyote aliye tayari kujiunga, lengo lao ni kuwahubiria Watanzania uzalendo ili kuleta amani na utulivu katika nchi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita ili kuonyesha uzalendo, wana kikundi hao walianza kwa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu hapa jijini Dar es Salaam kwa kuanza na mwandishi mkongwe, Athuman Hamis, ambaye alipata ajali alipokuwa kazini iliyomsababishia asiweze kusimama mwenyewe na kuendelea na shughuli zake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, alisema wameanza na Hamisi kama mfano na huo ndiyo uzalendo na wanaamini kila Mtanzania akiwa mzalendo nchi yetu itapiga hatua kimaendeleo.

“Mimi naamini tukiwa wazalendo basi hata matukio ya kupigana risasi na kutekwa yatatoweka, kwa maana haya yote yanatokana na kukosa uzalendo na sisi kama watu maarufu tumeliona hilo, ndiyo maana tumeamua kuanzisha kampeni hii ili kila mtu ajitambue kwa nafasi yake, lengo letu ni kumsaidia Mheshimiwa Rais, ambaye ni mzalendo namba moja anayepinga rushwa, unyanyasaji na mambo mengine yanayotaka kuliteketeza taifa,” alisema Steve Nyerere.

Aidha, pia aliwatambulisha baadhi ya wachezaji mpira wa zamani waliojiunga na umoja huo ulioazimia kutangaza uzalendo kwa kila rika, ambao ni Steven Nemes, Haji Ramadhani, Mwanamtwa Kiwhelu, Dotto Rutta ‘Mokili’ na wengine wengi.

Mbali na wachezaji mpira, baadhi ya wasanii maarufu pia walijiunga na umoja huo, wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wamelitumikia taifa kikamilifu na kutimiza ndoto zao, mmojawapo ni msanii Hellen Geogre ‘Rubby’, ambaye ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya.

Steve Nyerere aliongeza: “Tumempokea Rubby katika umoja huu kwa kuwa ameonesha nia ya kuutangaza uzalendo na tayari ameshatunga wimbo utakaohusu uzalendo ili kuongeza msisimko kwa jamii wafahamu uzalendo ni nini na muda si mrefu utaanza kusikika, pia tutautumia kama utambulisho wetu.”

Hata hivyo, Steve Nyerere aliweka wazi kuwa, timu hiyo ya uzalendo  imejipanga kuhakikisha wanazunguka nchi nzima kumwelimisha kila Mtanzania kujua nini maana ya uzalendo na utamsaidia nini yeye na vizazi vijavyo kama atakuwa mzalendo.

BINGWA lilifanikiwa kuzungumza na Rubby, ambaye alisema anaamini baada ya kuingia uzalendoni, basi ndoto zake zitatimia kwa kuwa hiyo ilikuwa ni hamu yake kubwa kuitangaza nchi yake.

“Namshukuru Mungu hii kauli mbiu ya uzalendo itanirudisha kwenye ramani na mashabiki wangu kujua mimi ni mzalendo ninayeipenda nchi yangu, siko tayari kuona taifa langu likiharibiwa na watu wachache, nitapigana hadi kuona kila mtu anakuwa mzalendo na niko tayari kuzunguka nchi nzima ili kuhakikisha nchi inakuwa ya kizalendo ili tuishi kwa amani,” alisema Rubby.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -