Saturday, October 31, 2020

RUBY ALIVYOITUMIA MISS TANZANIA KUIKUMBUSHA TANZANIA ‘WHO IS SHE’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MICHAEL MAURUS


KUNA msemo wa Kiingereza usemao ‘the first cut is the deepest one’ kwa tafsiri isiyo rasmi, ukimaanisha unapokata kitu kwa mara ya kwanza, kinaingia zaidi ya unapofanya hivyo kwa mara ya pili na zaidi.

Ufafanuzi zaidi ya msemo huo ni kwamba, inapotokea mtu anamchoma kisu mwenzake, kwa mara ya kwanza kitaingia zaidi kuliko itakavyokuwa kwa mara ya pili kwani atakuwa akifanya hivyo huku tayari akiwa na hofu au kujiona kama mkosefu.

Nini maana ya msemo huu katika maisha yetu ya kila siku? Ni hivi, unapotaka kufanya jambo lako kwa mara ya kwanza, usibahatishe. Ingiza nguvu, uwezo, akili na maombi yako yote ili ufanye kwa ufanisi.

Kwa mfano rahisi ambao utawagusa wengi. Kama wewe ni mwanaume, unapokutana na msichana unayempenda siku ya kwanza, hakikisha umejipanga vilivyo kushusha ‘nondo’ za nguvu kwani iwapo utachemka, utakapokutana naye mara ya pili (iwapo utabahatika), hutaweza kuwa na jipya mbele yake kwani u didn’t cut deeply at the first cut (mara ya kwanza hukukata barabara).

Hellen George, msanii wa kike anayetajwa kuwa na kipaji cha hali ya juu katika kuimba muziki, inaonekana anaufahamu vizuri mno msemo huo wa ‘the first cut is the deepest one’ kwani mara alipofahamu kuwa anatakiwa kufanya shoo katika jukwaa la Miss Tanzania 2018, hakutaka kufanya kosa hata kidogo.

Msanii huyo anayefahamika zaidi kwa jina la kimuziki la Ruby, alijipanga hasa ili aweze kukata barabara mara tu atakapopanda jukwaani katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam zilikofanyika fainali za mashindano hayo ya urembo nchini ambayo yalimshuhudia Queen Elizabeth Makune akibeba taji la Miss Tanzania 2018.

‘Kisu’ alichopanda nacho jukwaani ili kukata barabara kwa mara ya kwanza si kile kinachokatia vitunguu au nyanya, bali ni wimbo wa msanii mahiri wa Marekani, Beyonce unaokwenda kwa jina la Listen.

Kama lilivyo jina la wimbo huo, inawezekana Ruby alikuwa akitoa ujumbe kwa Watanzania akiwataka wamsikilize kubaini ubora wake ili kuacha kabisa kumfananisha na msanii mwingine yeyote hapa nchini.

Binafsi, namhusudu sana binti huyu kama ilivyo kwa Maunda Zorro, Mwasiti Almasi, mwanadada Pipi na wengineo wa aina yao ambao wamebarikiwa kuwa na sauti ya kimuziki hasa, lakini pia wakiwa na vipaji vya fani hiyo.

Mara alipopanda jukwaani na kuanza kuuimba wimbo huo wa Listen, kazi yake Beyonce, umati wa mashabiki wake, wadau wa urembo na wapenzi wa burudani kwa jumla, ulilipuka kwa shangwe wakimshangilia binti huyo, huku kelele zikizidi pale alipokuwa akicheza na sauti yake kuutendea haki wimbo huo.

Kati ya watu waliopagawishwa na Ruby usiku huo wa kuamkia Jumapili, ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ambaye ni miongoni mwa wadau wakubwa wa mashindano ya urembo na burudani kwa ujumla.

Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili 2006, lakini pia Balozi wa Redd’s wa mwaka huo, ni mmoja wa waimbaji wazuri mno ambaye wakati akiwa shuleni, pale St. Anthony, Mbagala, Dar es Salaam, alikuwa ni miongoni mwa wasichana waliokuwa wakitisha katika kuimba nyimbo za Kiingereza za wasanii wa Marekani na kwingineko, akibebwa na uwezo wake mkubwa wakuzungumza Kiingereza kwa mujibu wa mmoja wa walimu wake niliyekuwa ninaishi naye Keko Machungwa, jijini.

Kwa muda wote ambao Ruby alikuwa akiimba wimbo huo wa Listen, Jokate alikuwa amesimama akiuweka pembeni kabisa uheshimiwa wake kama kiongozi mkubwa kabisa wa Serikali wilayani Kisarawe, mkoani Pwani.

Jokate alionyesha wazi jinsi alivyoguswa na kipaji cha Ruby, lakini pia inawezekana ujumbe ulimo katika wimbo huo wa Listen, kazi yake Beyonce.

Mbali ya Jokate, mwingine aliyeguswa na Ruby kupitia wimbo wa Listen, ni Miss Tanzania 2004, Faraja Kota, ambaye naye muda wote alikuwa amepigwa na butwaa akimsikiliza binti huyo.

Hebu pata uhondo wa mashairi ya wimbo wa Listen wa Beyonce ambao ulimfanya Ruby kuuteka umati uliohudhuria fainali za Miss Tanzania usiku wa kuamkia Jumapili ya wiki iliyopita.

 

Listen to the song here in my heart

A melody I start but can’t complete

Listen to the sound from deep within

Its only beginning to find release

Oh the time has come for my dreams to be heard

They will not be pushed aside and turned

Into your own, all ’cause you won’t listen

Listen, I am alone at a crossroads

I’m not at home in my own home

And I’ve tried and tried

To say what’s on my mind

You should have known

Now I’m done believing you

You don’t know what I’m feeling

I’m more than what

You’ve made of me

I followed the voice, you gave to me

But now I’ve gotta find my own

You should have listened

There was someone here inside

Someone I thought had died

So long ago

Oh I’m screaming out

And my dreams will be heard

They will not be pushed aside or turned

Into your…

Katika wimbo huo, Ruby ni kama anawataka Watanzania kusikiliza uimbaji wake unaotoka moyoni mwake, akielezea jinsi alivyoanza muziki kwa kishindo, lakini kuna wakati alielekea kupotea. Anasema muda umefika wa kushamiri tena na kutimiza ndoto zake. Anasema anajiona kama yupo mpweke hivyo anahitaji sapoti ya wadau akiamini hakuna kama yeye.

Lakini vipi kwa Jokate? Naye wimbo huo unamgusa baada ya kipaji chake katika uongozi kuonekana na kupewa cheo alichonacho kwa sasa Kisarawe? Je, naye anawaambia Watanzania kuwa watarajie makubwa zaidi kutoka kwake? Je, naye ana ndoto ya kuwa kama Mama Samia Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania na hata Rais? Tusubiri tuone.

Baada ya kuimba wimbo huo wa Listen, Ruby aliendelea na nyimbo zake za ‘Na Yule’ wenye maneno ‘mapenzi hayana mwenyewe, unaweza kupenda kijana au mzee… na kuhitimisha shoo yake na wimbo wa ‘Niwaze’ aliolishirikisha kundi la The Mafik.

Ama kwa hakika, Ruby alifanikiwa mno kuunogesha usiku huo na kwa jinsi alivyozichanga karata zake kupitia msemo wa the first cut is the deepest one’, hata kama asingeimba nyimbo zake za ‘Na Yule’ pamoja na ‘Niwaze’, wimbo wa Listen pekee ulimtosha kuwakumbusha Watanzania ‘who is she’ (yeye ni nani) katika suala zima la muziki.

Msanii mwingine aliyeuwasha moto katika jukwaa hilo, alikuwa ni kijana anayetajwa kuwa na kipaji cha kuimba, lakini pia akiwa ni mtaalamu wa kupangilia muziki wake, Barnaba Elias ‘Barnaba’.

Kama ilivyo kawaida yake, Barnaba alitoa burudani ya nguvu, akibebwa na kujiamini kwake, ucheshi, utundu na kipaji chake cha kuimba, hasa muziki wa ‘live’.

Alianza na wimbo wake wa ‘Wrong Number’ aliomshirikisha Linah, ‘Tuachane Mdogo Mdogo’ na kumalizia na ngoma ‘Mapenzi Jeneza’ iliyopokewa vizuri mno na mashabiki.

Pia, kuna kipaji kipya cha Bongo Fleva anayekwenda kwa jina la Michael Muganda ‘Mycoel’ ambaye naye alifanya mambo makubwa mno kwa kuimba ‘live’ kuonyesha wazi Barnaba na wenzake wajipange hasa.

Mycoel, kijana mpole asiye na makeke, pamoja na wingi wa watu waliokuwapo ukumbini hapo, lakini akifahamu kuwa Barnaba na Ruby wanamtupia macho, hakuwa na mchecheto hata kidogo. Alifanya shoo ‘bab kubwa’ na kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani. Utapata nafasi ya kumfahamu zaidi msanii huyo katika toleo la BINGWA la Alhamisi hii.

Kwa ujumla, shoo ya Miss Tanzania 2018 ilikuwa ya aina yake, wapenzi wa urembo na burudani wakijitokeza kwa wingi mno tofauti na ilivyotarajiwa kuonyesha wazi kuwa mashindano hayo bado yana msisimko pamoja na changamoto kadha wa kadha zilizowahi kutokea.

Yote kwa yote, tusisahau ombi la Ruby, tumsikilize, kumwelewa na kumpa sapoti ili aweze kutimiza ndoto zake katika muziki.

Kama una lolote la kuchangia, karibu: 0713 556022

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -