Friday, January 15, 2021

RUFAA YA RONALDO YAGONGA MWAMBA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MADRID, Hispania

SHIRIKISHO la Soka nchini Hispania (RFEF), limeipiga chini rufaa iliyokatwa na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, kupinga kufungiwa kucheza mechi tano baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa kuwania Kombe la Supercopa de Espana dhidi ya Barcelona.

Ronaldo alipewa adhabu hiyo mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumsukuma mwamuzi katika mchezo ambao Real Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona wa kuwania Kombe la Supercopa de Espana ambao ulipigwa Jumapili iliyopita.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Mreno huyo alitokea benchi  na kisha akafunga bao ambapo alishangilia kwa kuvua jezi lakini dakika mbili baadaye akaongezwa kadi nyingine ya njano baada ya kujiangusha ndani ya eneo la hatari.

Kadi hiyo ndiyo iliyomfanya Ronaldo kushikwa na hasira na kujikuta akimsukuma aliyekuwa mwamuzi wa  mechi hiyo, Ricardo de Burgos.

Kutokana na kosa hilo, staa huyo mwenye umri wa miaka 32, alistahili kufungiwa kucheza mechi 12, lakini  RFEF wakamwonea huruma na kumfungia kucheza tano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na RFEF, mechi moja aliyofungiwa Ronaldo ni kutokana na kadi zile mbili na nyingine nne ni kwa ajili ya kitendo alichokionesha  dhidi ya mwamuzi huyo, De Burgos.

Mbali na adhabu hiyo, RFEF vile vile ilimlima faini  Ronaldo  ya Euro 3,850  na huku klabu yake nayo ikiadhibiwa kulipa faini ya Euro milioni 1,750.

Hata hivyo, Real Madrid ilipinga adhabu hiyo, lakini rufaa hiyo imetupiliwa mbali ambapo Ronaldo alilazimika kuikosa mechi ya usiku wa kuamkia jana ya marudiano  ya Kombe la  Supercopa, atazikosa za La Liga  ambayo itakuwa ugenini ikiumana na  Deportivo La Coruna na itakazokuwa nyumbani dhidi ya Valencia na  Levante na nyingine tena ya ugenini dhidi ya Real Sociedad.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -