Sunday, January 17, 2021

RUVU SHOOTING WANAONGOZA KWA WAHENGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA SALMA MPELI

WACHAMBUZI wengi wa soka wametabiri msimu huu wa Ligi Kuu Bara kuwa wa ushindani na utasisimua kutokana na timu zilivyojiandaa.

BINGWA linakuletea wastani wa umri wa timu zote 16 kwa mujibu wa taarifa walizowasilisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati wanapofanya usajili kuelekea msimu mpya.

Je, unajua timu gani ina wastani mkubwa wa umri wa wachezaji? Je, nani ni mchezaji mkongwe na kinda katika kila timu? Hii hapa ripoti kamili:-

Azam FC

Wanalambalamba hao wamesajili jumla ya wachezaji 27 wa kikosi cha wakubwa, huku beki kisiki wa kati, Aggrey Morris, akiwa mchezaji mwenye umri mkubwa ambapo rekodi zinaonyesha ana miaka 33, wakati Mghana Enock Atta Agyei ndiye mchezaji mwenye umri mdogo, akiwa na miaka 18. Wastani wa umri wa kikosi cha wakubwa cha Azam FC ni miaka 23.15.

Kagera Sugar

Timu hiyo yenye maskani yake mjini Bukoba, mkoani Kagera, ina wastani wa umri wa miaka 25.44 wa wachezaji wake wote 27 katika kikosi cha wakubwa.

Mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwenye kikosi hicho ni George Kavilla, ambaye ana miaka 38, huku Selemani Nyoni akiwa mchezaji mwenye umri mdogo, akiwa na miaka 19.

Lipuli FC

Wageni hawa wa Ligi Kuu Bara kutoka mkoani Iringa wamesajili wachezaji 28 ambao wastani wa umri wao ni miaka 24.36.

Katika kikosi hicho, mchezaji ‘mkongwe’ ni Hamad Manzi, mwenye miaka 29, huku Tola Mwangonela akiwa mchezaji mwenye umri mdogo, akiwa na miaka 20.

Majimaji FC

Wastani wa umri wa wachezaji katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya Wanalizombe kutoka Songea, mkoani Ruvuma ni 24.95.

Miaka 31 ndiyo umri wa mchezaji mkubwa katika kikosi hicho, ambaye ni Paul Maona, huku Six Mwasekaga, mwenye miaka 20, ndiye mchezaji mdogo zaidi.

Mbao FC

Timu hiyo yenye misimu miwili sasa katika Ligi Kuu Bara, imesajili jumla ya wachezaji 25, ambao wastani wa umri wao ni miaka 21.28.

Lakini mchezaji David Majinge Mwasa ndiye mwenye umri mkubwa, akiwa na miaka 26, na mwenye umri mdogo zaidi ni Habibu Kiyombo, mwenye miaka 19.

Mbeya City

Waite Wagonga Nyundo kutoka Mkoa wa Mbeya, ambapo wamesajili jumla ya wachezaji 26 kikosi cha wakubwa, kikiwa na wastani wa miaka 23.23.

Mbeya City inaongozwa na mchezaji Mohamed Samatta, mwenye umri wa miaka 29, huku Emmanuel Kakuti, mwenye miaka 19, akiwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi.

Mtibwa Sugar

Vincent Barnabas ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa, akiwa na miaka 32, huku Riffat Khamis akiwa mchezaji mwenye umri mdogo wa miaka 17.

Lakini wastani wa umri katika kikosi cha wakubwa cha Wakata Miwa hawa kutoka Turiani, Morogoro, iliyosajili jumla ya wachezaji 27, ni miaka 24.

Mwadui

Jumla ya wachezaji 20 ndio waliosajiliwa na timu ya Mwadui, ambapo wastani wa umri katika kikosi cha kwanza ni miaka 23.9.

Mchezaji Antony Matogolo, mwenye miaka 31, ndiye anayeongoza kwa ukongwe, wakati kinda katika kikosi hicho ni Razack Khalfan, mwenye miaka 18.

Ndanda

Timu hiyo yenye maskani yake mkoani Mtwara, ina wachezaji 27, ambao wastani wa miaka ya timu hii ni 22.96.

Mchezaji mwenye umri mkubwa kwenye kikosi cha wakubwa ni Jabir Aziz, akiwa na miaka 30, huku Ismail Aziz Kader akiwa mchezaji mwenye umri mdogo, akiwa na miaka 19.

Njombe Mji

Walibisha hodi Ligi Kuu Bara msimu huu na wakafunguliwa, ambapo waliwasilisha idadi ya wachezaji 28, huku kikosi cha wakubwa kikiwa na wastani wa miaka 22.82.

Mchezaji mwenye umri mkubwa ni Labani Kambole, mwenye miaka 29 na mdogo zaidi ni Mustapha Bakari, mwenye miaka 18.

Tanzania Prisons

Timu hiyo, inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini, yenye makao makuu yake mkoani Mbeya, ina jumla ya wachezaji 26, ambao wastani wa umri wa wachezaji wote hao ni miaka 25.23. Freddy Chudu ndiye anayeongoza, akiwa na miaka 33 na mwenye umri mdogo ni Japhat Meshack, ambaye ana miaka 19.

Ruvu Shooting

Wastani wa umri wa wachezaji wanaounda kikosi cha wakubwa cha Ruvu Shooting, yenye maskani yake mkoani Pwani, ni 26.34, ambayo inatokana na wachezaji 29 waliosajiliwa.

Shaibu Nayopa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi, akiwa na miaka 39, wakati Jamal Soud akiwa mchezaji mdogo zaidi wa miaka 20.

Singida United

Timu hiyo imepanda daraja msimu huu, ina wachezaji 26, ambao wastani wa miaka yao ni 24.23.

Kipa mzoefu, Ally Mustafa ‘Barthez’, anaongoza kwenye orodha ya wachezaji wenye umri mkubwa zaidi, akiwa na miaka 33, huku miaka 19 ni ya mchezaji Rolland Narsis Msonjo, akiwa ndiye mdogo zaidi.

Stand United

Kipa Frank Muwonge, mwenye miaka 30, ndiye mchezaji mkongwe katika kikosi cha wakubwa cha Stand United kilichosajili wachezaji 31.

Ikiwa na wastani wa umri wa miaka 21.24, David Mensah, mwenye miaka 18 ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi.

Simba

Timu hiyo kongwe nchini iliyosheheni wachezaji wa kigeni na wenye majina makubwa, ina wastani wa miaka 24.11 katika kikosi cha wakubwa.

Nahodha ambaye ni beki raia wa Zimbabwe, Method Mwajali, anaongoza kwa kuwa na umri mkubwa, akiwa na miaka 34, huku kinda Bukaba Bundala akiwa mchezaji mdogo mwenye miaka 19.

Yanga

Kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, kina jumla ya wachezaji 25 katika kikosi cha wakubwa ambapo wastani wa umri wao ni miaka 23.8.

Mchezaji mwenye umri mkubwa ni nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, akiwa na miaka 35, wakati beki Abdallah Haji Shaibu, maarufu Ninja, mwenye miaka 18, akiwa ni mchezaji mwenye umri mdogo zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -