Sunday, October 25, 2020

RUVU SHOOTING WATAJA  SABABU ZA KICHAPO

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MAREGES NYAMAKA

KOCHA wa timu ya Ruvu Shooting, Abdulmtuki Haji, ametaja sababu tatu za kukumbana na kipigo cha mabao 4-2 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mtanange huo ulikuwa wa tatu kwa Ruvu Shooting kufungwa kati ya michezo mitano waliyocheza tangu kuanza kwa Ligi Kuu Agosti 22, mwaka huu, huku pia wakiwa hawajaonja ladha ya ushindi.

Haji aliliambia BINGWA kuwa, wamekuwa na wakati mgumu katika michezo ya mwanzoni, kwani wamekuwa wanakumbana na changamoto kadhaa ambazo hata hivyo amedai kila kitu kitakaa sawa.

“Tatizo kubwa lilikuwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa mchezaji wetu na pia wachezaji wanane walibaki jijini Dar es Salaam kutokana na kuumwa na wengine tisa waliosafiri  hawakuruhusiwa kucheza kwa sababu hawakuwa na leseni,” alisema.

Aliongeza kuwa, wachezaji wengi waliokuwapo walitoka katika timu ya vijana, hivyo walilazimika kucheza nafasi ambazo hawajawahi kuzicheza, huku akisisitiza kuwa kwa uwezo wa Mungu mechi ijayo majeruhi watakuwa wamerejea.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -