Wednesday, November 25, 2020

Saa 48 hatari kwa Pluijm Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WAANDISHI WETU,

WAKATI Yanga wakicheza leo dhidi ya Kagera Sugar, kocha mkuu wa kikosi hicho, Hans van der Pluijm, kiroho kinamdunda kwani anaweza akatumbuliwa ndani ya saa 48 kuanzia sasa.

Unajua ikoje! Tayari kuna mipango ya chini kwa chini ya kumleta kocha mpya kutoka Zesco ya Zambia, George Lwandamina, ambapo ni kama Pluijm anatafutiwa sababu apigwe chini.

Wanachama wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kesho watakuwa na Mkutano Mkuu wa dharura ambapo unaweza ukatoka na maamuzi magumu kwa Pluijm.

Kama Yanga watapata matokeo mabaya katika mchezo wa leo kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera, hiyo inaweza kuwa fimbo ya kumchapia Pluijm.

Licha ya ukweli kwamba kuna idadi kubwa ya wanachama na mashabiki wanaomkubali Pluijm kutokana na kazi kubwa aliyoifanya hasa msimu uliopita, lakini imeonekana baadhi ya watu wa timu hiyo wamechochwa na Mholanzi huyo.

Taarifa za uhakika ambazo BINGWA linazo zinadai kuwa mazungumzo kati ya Yanga na kocha huyo mpya kutoka Zambia, yanaelekea pazuri hali ambayo inadhihirisha kuwa muda wowote Pluijm anaweza akaambiwa afungashe kila kilichochake.

Wanaotaka Pluijm aondoke wanadai kuwa Mholanzi huyo ni kama ameishiwa mbinu na sasa wanataka kocha mwingine ambaye atakuja na kitu kipya ambapo kura imemwangukia Lwandamina.

Pia taarifa hizo zinadai kuwa Pluijm aliambiwa aifikishe Yanga mbali katika michuano ya kimataifa, lakini wakatolewa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya pande hizo mbili.

Taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa Pluijm ataondoka na benchi lake zima akiwamo kocha msaidizi, Juma Mwambusi pamoja na Meneja wa kikosi hicho, Hafidh Saleh, ili kumpa nafasi huyo anayekuja aje na kikosi kazi kipya.

Wanaotajwa kuingia na kocha huyo mpya ni kocha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwassa, ambaye anaweza kuwa kocha msaidizi, huku Salvatory Edward akipigiwa chapuo kuwa meneja wa timu.

Katika mchezo wa leo, Pluijm anatakiwa kuzichanga vizuri karata zake ili kushinda na kuondoka na pointi zote tatu dhidi ya Wakata Miwa hao ambao nao wamepania kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani.

Msimu uliopita timu hizi zilipokutana Yanga waliibuka kidedea baada ya kushinda michezo yote miwili wakianza kushinda mabao 2-0, mchezo wa mzunguko wa kwanza Kagera wakiwa wenyeji Uwanja wa Kambarage na Wanajangwani hao wakashinda tena mabao 3-1 mzunguko wa pili Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo wa leo, Yanga itawategemea zaidi washambuliaji wake, Donald Ngoma pamoja na Obrey Chirwa ambaye ameanza kuonyesha cheche zake tofauti na alivyoanza.

Hata hivyo, Yanga hawatakiwi kuwadharau wapinzani wao hao kwani msimu huu wanaonekana kujipanga vizuri chini ya kocha wao, Mecky Mexime, ambaye walimchukua kutoka Mtibwa Sugar.

Katika hatua nyingine, wanachama wa Yanga, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika kesho katika makao ya klabu hiyo Jangwani kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo suala la ukodishwaji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa klabu hiyo, amesema kuwa mkutano huo utakuwa wa wazi na kila mwanachama atapewa nafasi ya kutoa maoni yake juu ya suala hilo.

“Mkutano utakuwa wa huru na haki na kila mwanachama atapata nafasi ya kutoa maoni yake juu ya mchakato huo wa mabadiliko. Nitatoka nje ili watu wapate uhuru wa kupiga kura,” alisema.

Akizungumzia sakata la Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali, Mwenyekiti huyo alisema mzee huyo hawezi kuhudhuria mkutano huo kwa kuwa si mwanachama.

“Kuna taarifa zinasema Akilimali si mwanachama kwa kuwa hajalipa ada kwa zaidi ya miezi sita sasa, hivyo kama anataka kuja kwenye mkutano afuate utaratibu wa kulipa ada,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema katiba ya klabu hiyo inasema mwanachama yeyote atakayekuwa hajalipia ada kwa muda wa miezi sita basi atakuwa amejifuta uanachama hivyo hata Akilimali anapaswa kuanza utaratibu upya wa kuomba uanachama.

“Akilimali anapaswa kwenda kwa mwenyekiti wake wa matawi ili aombe uanachama upya kwa kuwa sasa si mwanachama kutokana na kutolipa ada kwa miezi sita sasa,” alisema.

Akizungumzia suala lao la uwanja wa klabu hiyo, Mwenyekiti huyo alisema anatarajia kuanza kujenga uwanja ndani ya siku 90 katika eneo la Gezaulole lililopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Alisema kwenye eneo la Uwanja wa Kaunda uliopo kwenye makao makuu ya klabu hiyo ndio utajengwa uwanja mkubwa utakaotumika kwa ajili ya mechi.

“Ndani ya siku 90 zoezi linaanza rasmi hivyo kule Gezaulole kutajengwa uwanja wa mazoezi na hapa Kaunda ndio uwanja mkubwa ila mipango yetu ni mara.

“Ni kweli kuna mgogoro, lakini haujagusa eneo lote, eneo lenye mgogoro ni ekari 30 tu ila tayari tumeshapeleka barua kwa mkuu wa Wilaya ya Ilala, ili waweze kutatua suala hilo kabla hatujaanza ujenzi,” alisema.

Kuhusu tetesi kuwa anakusudia kuitema Yanga, alisema: “Siwezi kuiacha Yanga ila maamuzi yatakayotoka kwenye mkutano, ndiyo yatakayotoa mwelekeo.”

Habari hii imeandaliwa na HUSSEIN OMAR, EZEKIEL TENDWA NA ZAITUNI KIBWANA.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -