Tuesday, November 24, 2020

SABABU TANO KUTIMULIWA KWA HANS PLUIJM

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MKURUGENZI wa Ufundi wa Yanga, Hans van der Pluijm, ametimuliwa katika nafasi hiyo, huku sababu za kuvuliwa cheo hicho zikitajwa.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana, zinasema ukata ni moja ya sababu zilizochangia Yanga kufikia uamuzi wa kumtema Pluijm, uliofanywa na viongozi wa timu hiyo waliokutana kwa siri jijini, lengo likiwa ni kupunguza matumizi.

“Jana kulifanyika kikao cha baadhi ya viongozi na kufikia uamuzi huo ambao umefanywa kwa maslahi ya pande zote mbili, yaani mwalimu na klabu,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakupenda jina lake kuwekwa hadharani, kwa madai kuwa hana mamlaka wa kulizungumzia hilo.

Alisema kuwa, kuna mambo mengi yaliyochangia uamuzi huo, ikiwamo tabia zake, kwani kuna wakati ameonekana kuendekeza mambo madogo madogo. “Huwezi amini, hata posho kuna wakati huwa anashinikiza awe kwenye mgawo wakati hakupaswa kupewa, ukizingatia analipwa mshahara mkubwa zaidi ya mtu yeyote kwenye benchi la ufundi,” kilisema chanzo hicho.

Lakini pia, inadaiwa kuwa Pluijm ameonekana kutoridhishwa na kitendo cha kuporwa nafasi yake na Kocha Mkuu George Lwandamina, hivyo kufanya mikakati ya chini kwa chini kuhakikisha mwenzake huyo anafeli.

Chanzo cha kuaminika kimeliambia BINGWA kuwa, Mholanzi huyo amewateka baadhi ya wachezaji ili kusambaza ‘sumu’ kwa wenzao, lengo likiwa ni kumharibia Lwandamina.

Katika hilo, Pluijm anadaiwa kujifanya mtetezi wa wachezaji katika masuala mbalimbali, ikiwamo posho na nafasi ya kucheza, wengine wakiwa ni wale ambao yeye hakuwa akiwapa nafasi.

Kati ya mbinu anazodaiwa kuzitumia Pluijm kumchafua Mzambia huyo ni kuwa karibu zaidi na wachezaji na kuzungumza nao kwa muda mrefu, lengo likiwa ni kuwafanya waamini yeye bado ni lulu Jangwani.

Lakini pia, mwanzoni mwa mwaka huu, ilidaiwa kuwa Pluijm alishinikiza baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kugomea mazoezi, wakiushinikiza uongozi wa timu hiyo kuwalipa mishahara.

Akiwa kama Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm amekuwa akionekana kutoshitushwa na matokeo mabaya wanayoipata timu hiyo kama ilivyojionesha katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Simba, ambapo akiwa nje ya uwanja alionekana akitabasamu, huku akikataa kuhojiwa na waandishi wa habari.

BINGWA lilimtafuta Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, kulizungumzia hilo ambapo alisema: “Hizo ni habari ambazo zipo kwenye mitandao, hazijawa rasmi, nikiwa kama mtendaji mkuu wa klabu, zikiwa rasmi nitawafahamisha.”

Kwa upande wake, Pluijm alisema: “Nimepokea barua leo asubuhi baada ya mazoezi ikionyesha kuwa nimesitishiwa mkataba na timu, huku tatizo kubwa likitajwa kuwa ni hali ya kifedha. Muda si mrefu nitatoa mwelekeo wangu kuwa ninaelekea wapi na kuangalia jinsi gani nitapata maslahi yangu.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -