Tuesday, December 1, 2020

Sababu tano kwanini huu ni mwaka wa Liverpool?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MERSEYSIDE, England

KLABU ya Liverpool haijabeba taji la Ligi Kuu England tangu mwaka 1990, lakini msimu huu wameanza vizuri baada ya kukusanya pointi 23 katika mechi 10 walizocheza.

Mchambuzi wa Sky Sports, Phil Thompson, ameainisha sababu tano kwanini huu ni msimu wa Liverpool kunyakua taji hilo la Ligi Kuu England.

 

  1. Majeruhi

Majeruhi yana nafasi kubwa kwenye kunyakua taji. Tuliona Leicester City msimu uliopita, jinsi walivyoweza kuepuka majeruhi ndivyo walivyoweza kufanya vizuri.

Kwa upande wa wachezaji muhimu wa Liverpool wakifanikiwa kuwa fiti, basi kila kitu kitakwenda vizuri. Wachezaji hao muhimu ni katika safu ya ushambuliaji Firmino, Coutinho, Mane, Lallana na Sturridge. Wanahitaji kuepuka majeruhi na kuweza kuwazidi wapinzani wao. Wachezaji hao wote watano ni muhimu sana kwa sasa.

 

  1. Kiwango cha nyumbani

Kiwango chao kwenye uwanja wa nyumba ni muhimu sana. Kiwango kizuri kwenye uwanja wa nyumbani ni jambo la msingi na ndio kitu ambacho kiliweza kuwasaidia Liverpool na Manchester United kwa kipindi kile walichokuwa wanafanya vizuri.

Ukiwa na uhakika wa kushinda nyumbani na kujua namna ya kushughulika na mechi za ugenini usifungwe, utakuwa kwenye wakati mzuri.

Kiwango cha soka cha nyumbani cha Liverpool hakikuwa kizuri katika miaka iliyopita, lakini sasa Jurgen Klopp ameanza kulifanyia kazi jambo hilo.

Ndio maana kuna mabadiliko yanaonekana kwa upande wa mechi za nyumbani na nina uhakika kwa kocha huyo atahakikisha kwamba anaifanya Anfield kuwa sehemu tishio.

 

  1. Liverpool wanatakiwa kushinda mechi wanazopaswa kushinda

Hilo linaweza likawa jambo rahisi, lakini unapoliangalia hilo, Liverpool wamekuwa wakishughulika na mechi ngumu, wanaonekana kushinda mechi kubwa pekee.

Timu inaonekana kushinda mechi ngumu kuliko mechi kama Newcastle, Watford, Swansea haswa kwenye msimu ulipita. Wamekuwa wakifungwa kwenye mechi ndogo na kushinda mechi kubwa.

Lakini Jurgen anaonekana kulitatua tatizo hilo ambalo ni moja ya jambo kubwa sana lililokuwa likihitaji kufanyiwa kazi mwanzoni mwa msimu.

 

  1. Kulinda mipira ya adhabu

Mambo yamekuwa mazuri na ni muhimu sana kwamba wameanza kulifanyia suala hilo kazi kwenye mazoezi. Jurgen Klopp ametambua hilo na wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanatatua tatizo hilo pamoja na mlinda mlango wao, Loris Karius, kwa sababu wanajua kwamba Ligi Kuu England wachezaji wote wanakusanyika kwenye boksi dogo na hufanya kazi ya kujilinda kuwa ngumu kwa mabeki.

Wanapaswa kuwa makini kwa kiwango kikubwa mno ili kuweza kuepusha hatari ambazo zinaweza kujitokeza na kuweza kufanyia kazi matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kila mara. Kama watafanikiwa kufanya hivyo mara zote kwenye mipira ya adhabu, basi nafikiri watakuwa vizuri na hayo ni mambo ambayo yatawapa ubingwa kwa kuwa watakuwa wakikusanya pointi na kuepuka kufungwa kwa urahisi.

Kama unakumbuka kipindi mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea, anawasili kwenye klabu hiyo ya Old Trafford, walikuwa wakifanya mambo sawa na yale wanayomfanyia kipa huyo wa Liverpool, Karius. Lakini mlinda mlango huyo, De Gea ameweza kujifunza na Karius anapaswa kufanya hivyo.

 

  1. Kocha

Klopp ni bonge la kocha, mwenye ushawishi, anaaminika na kila mmoja; mashabiki, wachezaji, anaonekana kufanya vizuri akiwa na wachezaji wake.

Wanaweza kujiandaa na mechi, wanapata muda wa kutosha kupumzika na unaweza kuliona hilo katika uwanja wao wa Anfield kwenye mechi za nyumbani. Yeye ni mmoja ya watu muhimu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -