Wednesday, October 28, 2020

SABABU TATU ZA WENYEJI GABON KUONDOLEWA MAPEMA AFCON

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LIBREVILLE, Gabon

USIKU wa Jumapili ya wikiendi iliyopita, kikosi cha timu ya taifa ya Gabon kilikuwa ni cha kwanza kutolewa hatua ya makundi ya Afcon, baada ya kulazimishwa suluhu na Cameroon, ambapo mara ya mwisho kwa mwenyeji kutolewa hatua hiyo ni Tunisia mwaka 1994.

Unajua sababu zilizosababisha wenyeji hao wanaoongozwa na nahodha wao mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang? Hizi hapa sababu tatu za msingi:

Pierre-Emerick Aubameyang

Straika huyo alifanya kazi kubwa kuliko wenzake hadi walipoondolewa mashindanoni.

Unaweza ukajiuliza ni kazi gani kubwa aliyoifanya? Mabao mawili tu?

Ni maswali makali mno kwani kama ulikitazama kiwango chake pale Gabon, utagundua si mtu wa ‘levo’ sawa na wenzake. Angefanya lipi jingine zaidi ya lile?

Kwenye mtanange wao dhidi ya Cameroon alikosa bao la wazi ambalo lingebadili hali ya hewa pale. Pia hakuonekana kama ni nahodha tena, hakuibeba timu mgongoni mwake tena, hayo yasikusumbue sana.

Aubameyang alichoka, kuanzia uwanjani hadi ndani ya timu kwa ujumla. Kikosi hakikupata muda wa kutosha wa kujiandaa (kwa mujibu wake). Vyote vilimchosha na kumsababishia uchovu wa akili na mwili.

Kila mtu alitamani kumwona nahodha huyu akirudi chini kuisaidia timu pindi mambo yanapokuwa magumu, badala ya muda wote kuutumia akiwa kwenye eneo lake la ushambuliaji licha ya upungufu wa huduma za viungo ndani ya kikosi chake hicho.

Si kila nahodha ana uwezo wa kuongoza timu ila Aubameyang hakuwa na budi zaidi ya kutimiza jukumu. Hata hivyo, kwa uchovu aliokuwa nao, mabao yake mawili dhidi ya Guinea-Bissau na Burkina Faso yalikuwa na thamani katika safari ngumu ya Gabon.

Kikosi cha Gabon

Aubameyang hakung’ara lakini kuondolewa kwa Gabon kulidhihirisha namna walivyokuwa dhaifu kama timu kwa ujumla, ambapo udhaifu wao hasa ulikuwa ni kwenye kiungo cha kati kwani walikosa mtu aliyekuwa na uwezo wa kumiliki mpira na kuifanya timu iwe na uwiano mzuri.

Kiungo Mario Lemina anayekipiga Juventus, alijaribu kucheza vema kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Guinea-Bissau uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, lakini kadiri mchezo ulivyoendelea, alipotea kabisa na labda ubovu wa kiwanja cha de L’Amitie nao ulichangia hilo.

Aidha, Lemina alipoumia na kuondolewa kwenye kikosi cha Gabon, timu hiyo ilikosa mtu ambaye angalau angewasaidia kuunda mashambulizi kwa utulivu.

Mipira mingi mirefu isiyokuwa na faida ilianza kupigwa kwa Aubameyang, naye alihangaika kuifuata kwa kasi huku akiitazama ikitoka nje.

Kikosi kizima cha Gabon kilishindwa kuonesha upinzani mkali dhidi ya wapinzani wao wa kundi. Walishindwa kucheza soka lao dhidi ya Cameroon na Burkina Faso waliocheza soka la nguvu na kasi.

Safu yao ya ulinzi pia haikutulia, kila kitu ndani ya kikosi cha Gabon hakikuwa na uwezo wa kufanya yale yaliyokuwa mawazoni mwa wadau wa soka.

Mashabiki wa Gabon

Mchezaji wa 12 ni muhimu mno kwenye soka. Wakati Jose Mourinho akiwalilia mashabiki wake kuhusu suala la mashabiki wake pale Old Trafford kuishangilia timu kadiri wawezavyo, hali ilikuwa ni tofauti pale Stade de L’Amitie, Libreville.

Hakukuwa na hamasa ya kutosha kutoka kwa mashabiki, viti vingi uwanjani vilikuwa vitupu. Ni kama vile Gabon ilikuwa ugenini. Haikupata upendo wa kweli kutoka kwa mchezo wao wa 12.

Tofauti na ilivyokuwa Afcon iliyofanyika Guinea ya Ikweta miaka miwili iliyopita, mashabiki wa timu mwenyeji walifurika jijini Bata na kuishangilia mno timu yao. Kelele zao ziliwasisimua wapinzani, kelele hizo pia ziliwasukuma vijana wao hadi robo fainali na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tunisia.

Timu wenyeji siku zote huwa zinapata hamasa ya kufanya vizuri kutokana na uzalendo wa mashabiki wao hasa wanapokuwa na furaha ya kuiona nchi yao ikiwa mwenyeji wa michuano mikubwa; kwa nchi ya Gabon, mashabiki wao walionekana kuwa na matatizo yao wenyewe yaliyowasumbua akilini mwao na hawakuwa na hamu yoyote ya kuwapa sapoti wachezaji wao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -