Friday, November 27, 2020

SABABU TISA ZINAZOMTOA FELLAINI KIKOSI CHA KWANZA UNITED

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England


NDANI ya wiki hii nzima mchezaji anayezungumzwa sana miongoni mwa wadau wa soka ni kiungo wa klabu ya Manchester United, Marouane Fellaini.

Mbelgiji huyu anayejulikana zaidi kutokana na wingi wa nywele zake kichwani, umbo refu linalomfanya afanane na mti wa mnazi, kwa sasa anachukiwa zaidi pale Manchester kutokana na kitendo chake cha kuisababisha timu hiyo kupoteza pointi mbili za muhimu dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa wikiendi iliyopita.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho, alisema aliamua kufanya mabadiliko ya kumwingiza Fellaini kipindi cha pili kwa ajili ya kupunguza madhara ya mipira mingi mirefu iliyokuwa ikipigwa na Everton katika mchezo huo.

Lakini tofauti na kile ambacho kocha wake huyo alikitegemea, dakika chache baada ya Fellaini kuingia alijikuta akiwazawadia Everton penalti wakati huo United ikiongoza kwa bao 1-0! Ulimwengu mzima wa mashabiki wa United ulipatwa na ukimya wa ghafla kwani tayari walishaanza kufurahia pointi tatu.

Hizi ndizo sababu tisa zinazofafanua ni kwa namna gani Fellaini asivyo na faida ndani ya kikosi cha United.

Mosi, Mourinho kwa sasa anaonekana kuwa na machaguo ya kutosha kwenye safu yake ya kiungo. Ana Paul Pogba, Ander Herrera, Michael Carrick. Hata Morgan Schneiderlin au Bastian Schweinsteiger pia ni wachezaji bora kwenye eneo hilo wakati huo pia anaweza kuwatumia watu kama Juan Mata na Henrikh Mkhitaryan.

Pili, Jamaa anapenda sana kucheza rafu kwani takwimu zinasema kuwa tangu atue United mwanzoni mwa msimu wa 2013/14, amecheza rafu nyingi kuliko wachezaji wote kwa wakati huo (rafu 216). Na cha kushangaza anacheza rafu hizo huku akiwa hana namba ya kudumu kikosini, anawapiga wapinzani viwiko, hajui wapi pa kucheza rafu na wapi atulie.

Tatu, anapenda kupiga pasi nyingi zisizo na faida. Hadi sasa Fellaini amekamilisha jumla ya pasi 2,555 akiwa ndani ya jezi ya United katika michezo ya Ligi Kuu England na pasi 1,327 tu zimeisaidia United isukume mashambulizi (asilimia 51) wakati huo huo Michael Carrick amekwishapiga jumla ya pasi 2,931 na asilimia 70 ya pasi hizo zimeisaidia United kwa kiasi kikubwa kusukuma mashambulizi yao.

Nne, licha ya kuwa na uwezo wa kucheza kwenye eneo lolote la kiungo, Fellaini bado hajaweza kulimiliki vizuri eneo hilo (hasa kwenye suala la kupokonya mipira), kwani tangu alipotua United 2013, Mbelgiji huyo amepokonya mipira mara 116 wakati Ander Herrera aliyejiunga 2014 na kucheza michezo michache tayari amepokonya mipira mara 110.

Tano, licha ya urefu wake wa futi 6’4 kutazamwa kama ni faida kwa timu hasa kwenye michezo yenye kuhitaji wachezaji warefu kuzuia mipira ya juu, Fellaini hajaonesha uwezo wake huo kwa kiasi cha kutosha.

Amejaribu kuicheza mipira 238 akiwa na United kwenye ligi tofauti na Chris Smalling aliyempiku kwa kucheza mipira 269 tangu msimu wa 2013/14. Na kati ya mpira hiyo, Fellaini amefanikiwa kuicheza kwa asilimia 57 tu. Bado sana!

Sita, jamaa hafungi mabao ya kutosha tangu aliposajiliwa. Ndani ya miaka yake mitano ya kuichezea Everton, Fellaini alifunga mabao 25 na wakati huo alikuwa akichezeshwa kama kiungo mshambuliaji au straika, sasa ni nini kilichowafanya United wapendezwe naye?

Hadi sasa, Fellaini amefunga mabao saba ya ligi; sita kati ya hayo amefunga msimu wa 2014/15 kuanzia Desemba 12, 2015 hajafunga tena hadi leo!

Saba, hakuna kocha aliyeonekana kumwamini. Jamaa hadi sasa ameanza na kumaliza kwenye mechi 34 tu za ligi tangu ajiunge na klabu (asilimia 26 ya mechi 128 alizoichezea United).

Fellaini hajawahi kuwa mchezaji muhimu wa United na hatawahi kuwa na umuhimu huo!

Nane, Fellaini ana moto sana uwanjani. Unaweza kuamini kwamba jamaa ameoneshwa jumla ya kadi 15 tangu asajiliwe? Wakati nahodha wake ambaye yupo hapo kwa muda wa takribani miaka 10, Wayne Rooney, ana kadi 22.

Kwa aina ya rafu zake za viwiko hakuna kocha atakayemwamini hasa kwenye mechi zenye presha ya hali ya juu.

Tisa na mwisho, Fellaini kuna faida gani kwa United kuendelea kukaa na mtu ambaye pindi anapocheza tangu mwanzoni mwa msimu wa 2015/16, wanapata asilimia 34.4 ya ushindi lakini asipokuwapo wanapata asilimia 60.8 ya ushindi?

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -