Tuesday, October 27, 2020

SABABU YA ROBBEN KUTIMKA MADRID HII HAPA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MUNICH, Ujerumani


NI mmoja kati ya mastaa wakubwa kwenye kikosi cha sasa cha Bayern Munich. Hapa namzungumzia ‘fundi’ Arjen Robben.

Makeke yake anapokuwa uwanjani yamemfanya kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Winga huyo wa kimataifa wa Uholanzi alijiunga na miamba hiyo ya Bundesliga wakati wa majira ya kiangazi na hiyo ilikuwa mwaka 2009.

Wafuatiliaji wa soka la Ulaya, walianza kumjua mchezaji huyo akiwa na PSV katika msimu wa 2002-03.

Msimu mmoja baadaye alijiunga na wababe wa Stamford Bridge na kisha akasajiliwa na Real Madrid kabla ya kutua Ujerumani.

Mpaka sasa Robben ameshaipa Bayern mafanikio makubwa ikiwamo mchango wake wa mabao na ‘asisti’ kuwawezesha kunyakua mataji ya Bundesliga, La Liga na Kombe la Ligi.

Bayern wamefaidika na huduma ya Robben huku ikikumbukwa kuwa walitumia kiasi kidogo cha fedha cha euro milioni 25 kumnasa akitokea Madrid.

Hata hivyo, imefichuka kuwa Madrid hawakutaka kumuuza winga huyo na kilichosababisha hilo kutokea ni uhitaji mkubwa wa fedha waliokuwa nao mabingwa hao wa ligi kuu nchini Hispania ‘La Liga’.

Kwa mujibu wa Mholanzi huyo, Madrid hawakutaka kumpiga bei ila walilazimika kufanya hivyo kwa lengo la kuingiza fedha.

Alisema wala hakuwa na mpango wa kujiunga na Bayern, lakini baada ya Florentino Perez kurejea kwenye wadhifa wake wa urais, alitaka kuimarisha uchumi wa Madrid na njia sahihi ilikuwa ni kuwauza wachezaji ambao wangeipatia timu hiyo fedha nyingi.

“Tuliambiwa kuwa klabu ingeingiza fredha nyingi kwa kuniuza, lakini mwanzoni nilikataa kuondoka,” alisema Robben mwenye umri wa miaka 32.

Aidha, nyota huyo alikiambia kituo cha televisheni cha Fox Sports kuwa alifurahia maandalizi ya msimu wa 2008-09 akiwa Bernabeu, lakini alishangaa kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao mara 11 wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

“Nilikuwa na maandalizi mazuri ya msimu, sikupata nafasi kikosini, hivyo niliamua kufanya uamuzi.

“Ilikuwa ngumu pale Florentino Perez aliporejea madarakani na pia wachezaji wapya walipowasili,” alidai Robben.

Robben amekiri kuwa ujio wa mastaa Cristiano Ronaldo, Kaka, Karim Benzema na Xabi Alonso kuliifanya timu hiyo kutumia fedha nyingi kwenye soko la usajili.

Akilizungumzia hilo kwa mapana, amedai kuwa hakuwa na nafasi ya kuingia uwanjani mara kwa mara ingawa pia hakutamani kuondoka kwenye klabu hiyo ya jijini Madrid.

Aliongeza kuwa ilikuwa ngumu kutua Bayern kwa kuwa kwa kipindi hicho haikuwa miongoni mwa timu kubwa na tishio barani Ulaya.

Ikumbukwe kuwa, kipindi hicho anachokizungumzia Robben, Bayern hawakuwa wametinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa miaka nane mfululizo.

“Yalikuwa maamuzi magumu, magumu kuliko yote niliyowahi kuyafanya katika maisha yangu ya soka,” alisema.

“Bayern hawakuwa moja kati ya wababe wa Ulaya kwa kipindi kile (mwaka 2009). Kwangu ilikuwa ni kama kujirudisha nyuma.”

Ingawa Robben alihisi asingewika Ujerumani, alijikuta akiwa dhahabu nchini humo hasa kwa mafanikio ya haraka aliyopata akiwa na wakali hao wanaotumia Uwanja wa Allianz Arena.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa katika msimu wake wa kwanza akiwa na ‘uzi’ wa Bayern, Robben alikuwa sehemu ya kikosi hicho kilichofika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini pia, katika msimu wa 2012-13, aliiongoza timu hiyo kunyakua ubingwa wa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya ka ngazi ya klabu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -