Friday, December 4, 2020

SABABU ZA GUARDIOLA KUFUNIKWA NA CONTE LIGI KUU ENGLAND

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

JUMATANO ya wiki hii, Chelsea walikoleza mbio zao za kuufukuzia ubingwa baada ya kuwafunga Manchester City mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka, akiwamo Adam Bate, wanaamini kocha wa Chelsea, Antonio Conte, alimfunika vibaya mwenzake wa Man City, Pep Guardiola.

Si tu katika mtanange huo, wachambuzi wamedai Conte amekuwa akimpiku Guardiola tangu kuanza kwa msimu huu.

Licha ya ukweli kwamba vita kali ilitarajiwa wakati makocha hao wanatua England wakati wa majira ya kiangazi, tayari Guardiola ameonyesha kushindwa kuhimili vishindo vya Muitalia huyo.

Kwa upande mwingine, Guardiola alipewa nafasi kubwa mbele ya Conte kutokana na mataji aliyochukua akiwa na timu za ligi tofauti.

Ni tofauti na Conte, ambaye alichukua mataji matatu akiwa Italia pekee, tena akiwa na Juve tu.

Lakini pia, kilichowaaminisha wengi kuwa Guardiola angewika mbele ya Conte ni jinsi ambavyo Muitalia huyo aliikuta Chelsea, ambapo ilitoka kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 10.

Kwa ushindi ule wa mabao 2-1, Conte amekuwa kocha wa kwanza kumfunga mara mbili Guardiola katika msimu mmoja.

Sababu kubwa inayotajwa kuchangia Conte kumfunika Guardiola ni kiwango kizuri cha wachezaji wa Blues msimu huu.

Eden Hazard amekuwa kwenye kiwango kizuri na alipachika mabao yote mawili wakati Chelsea walipoisambaratisha Man City.

Idadi kubwa ya mabao ya Hazard msimu huu ni yale aliyofunga dhidi ya timu zinazoshika nafasi za juu kwenye ligi.

Arsenal, Everton, Manchester United, ni miongoni mwa timu zilizochangia mabao 13 ya Mbelgiji huyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Opta, Man City wamefunga mabao tisa pekee kati ya nafasi 26 za wazi walizopata katika mechi dhidi ya timu kubwa.

Mlinda mlango wa Man City, Willy Caballero, amekuwa akifanya makosa mengi na hata katika mtanange dhidi ya Chelsea alimzawadia Hazard bao la kuongoza.

Caballero, mwenye umri wa miaka 35, ameonekana kushindwa kuendana na presha ya timu inayosaka ubingwa.

Ujio wa Claudio Bravo haujazaa matunda, licha ya kuwa kipa ghali zaidi Ligi Kuu England.

Usajili wa David Luiz ulikosolewa vikali, lakini umeonekana kuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha Conte, huku N’Golo Kante akiendelea kutema cheche zake katika eneo la kiungo.

Lakini pia, tayari Conte ameonekana kuuimarisha mfumo wake wa 3-4-3 na wachezaji wameanza kuuzoea. Chelsea wametumia style hiyo ya uchezaji katika michezo 22 ya msimu huu.

Lakini, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mtandao wa Opta, mpaka sasa ni kama Guardiola hajapata mfumo rasmi.

Kocha huyo aliyewahi kutamba akiwa na Barcelona na Bayern Munich, ameshatumia mifumo saba tofauti tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Mwanzoni mwa msimu huu, Chelsea walishinda mechi sita wakiwa na kikosi kimoja, lakini Guardiola amekuwa akibadilisha wachezaji katika kila mchezo.

Tayari Guardiola ameshaonyesha dalili za kushindwa, hasa kwa kauli yake hivi karibuni kuwa anatarajia mabadiliko makubwa msimu ujao.

“Msimu ujao mambo yatakuwa mazuri. Miaka miwili itakuwa poa. Nipeni muda,” alisema Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 45.

Mbali na hilo, Guardiola ametilia shaka uwezekano wa kikosi chake kuchukua taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Kwa upande wake, Conte amefanikiwa kufanya mapinduzi makubwa Stamford Bridge na huenda akawapa taji msimu huu.

Amesisitiza kuwa kinachomnyima raha kwa sasa ni kushindwa kuwasiliana vizuri na wachezaji wake, kwani bado hajaweza kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiingereza.

Kutokana na hilo, amedai kuwa amekuwa akishindwa kuwahamasisha vizuri mastaa wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -