Sunday, January 17, 2021

Sababu za Pluijm kujiuzulu Yanga

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MWANDISHI WETU,

HANS van der Pluijm ameandika barua ya kijiuzulu kama kocha wa Yanga, ikiwa ni siku moja baada ya George Lwandamina anayeinoa Zesco ya Zambia kutua nchini tayari kubeba mikoba yake.

Akizungumza na BINGWA jijini Dar es Salaam jana jioni, Pluijm alikiri kuukabidhi uongozi wa Yanga barua ya uamuzi wake huo.

Japo kocha huyo raia wa Uholanzi alikataa kusema kwanini amechukua uamuzi huo, BINGWA linafahamu kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kumleta Lwandamina bila kumshirikisha, kimeonekana kumkera.

Pluijm alisema anaachia nafasi yake katika timu hiyo aliyoipa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara misimu miwili mfululizo, huku kukiwa na ofa nyingi mezani kwake.

“Nimekabidhi barua ya kujiuzulu na nipo tayari kufundisha popote ukizingatia kuwa kuna ofa nyingi mezani,” alisema.

BINGWA linafahamu kuwa tayari Pluijm ameanza mazungumzo na Azam na kwamba inadaiwa kuwa viongozi wa timu hiyo walionekana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, kwenda kumpokea alipowasili jijini akitokea mkoani Kagera ambako kikosi chake kilivaana na Kagera Sugar Jumamosi iliyopita na kushinda mabao 6-2.

Mapema jana, Pluijm alizungumza na BINGWA na kusema kuwa siku zote mlango mmoja ukifungwa, mingine hufunguka na kwamba kwa uzoefu alionao kwenye soka la Afrika na mchango mkubwa alioutoa kwa klabu nyingine, ana uhakika mkubwa kupata timu wakati wowote.

Alisema kimsingi hana tatizo juu ya ujio wa Lwandamina na kusisitiza kuwa amejifunza mengi katika kipindi chote alichofanya kazi akiwa na Yanga, huku akijivunia rekodi nzuri aliyoiacha kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Wanaweza kumleta wanayemtaka. Nimejifunza kitu kwa kipindi chote nilichofanya kazi na timu na wafanyakazi wa hapa. Hakuna anayeweza kupinga kuwa nimeweka rekodi hapa. Kama uongozi unataka mabadiliko ni juu yao,” alisema Pluijm.

“Hakuna jambo linaloshindikana mbele ya Mungu, kila kitu kinawezekana na ninaamini Mungu yupo nasi atafungua milango mingine,” alisema Pluijm.

Kutokana na kuzinasa taarifa hizo, BINGWA liliwasiliana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, kupata ukweli juu ya taarifa hizo.

Kawemba alidai kwa sasa hawana mpango na kocha huyo kwa sababu benchi lao la ufundi lipo kamili na wanaamini baada ya muda kikosi chao kitarudia makali yake ya misimu iliyopita.

Mtendaji huyo alisema nafasi ya kocha siku zote ni moja na tayari wana kocha wao na hawajawahi kufikiria kumchukua Pluijm kwa sababu hata akienda kwenye timu hiyo hawana pa kumweka.

Yanga imefikia uamuzi huo wa kuachana na Pluijm baada ya kuona timu yao ikiwa imeshuka kiwango na hivyo kuhofia huenda wakashindwa kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -