Thursday, October 22, 2020

Sababu za Ronaldo kuanza majukumu akiwa mdogo

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Madrid, Hispania

MALEZI ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, yalikuwa na changamoto nyingi na yalihitaji uvumilivu ambao leo unamlipa na anafaidi matunda yake.

Mchezaji huyo wa Ureno aliyezaliwa kitongoji cha Santo Antonio katika kisiwa cha Madeira, alipewa jina la ‘Ronaldo’ ambalo ni jina la Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, kwa kuwa baba yake mzazi, Jose Dinis Aveiro, alikuwa akimpenda kiongozi huyo.

Ronaldo ambaye utotoni alipewa jina la ‘Crybaby’ na wenzake kutokana na kupenda kulialia, alipitia changamoto nyingi na alianza majukumu ya kuwa baba akiwa na umri mdogo kutokana na baba yake kuwa mlevi kupindukia.

Pamoja na kuwa na ndugu zake kama kaka yake Hugo na dada zake wawili, Elma na Liliana Catia, lakini Ronaldo ndio alionekana kuihudumia familia yake akiwa mdogo.

Malezi

Baba yake Ronaldo, Aveiro ambaye alistaafu Jeshi la Ureno, alianza kufanya kazi za mitaani ili kuitunza familia yake, ambapo alifanya kibarua cha kutunza bustani za mji wa Madeira na uwanja wa soka wa Halmashauri ya Manispaa ya Madeira.

Jukumu lake kubwa kwenye uwanja huo lilikuwa ni kuutunza uwanja huo kwa kuokota taka, kusafisha vyoo, kutunza mipira na kuandaa vifaa vya mazoezi kabla ya makocha hawajaanza kuwafunza soka watoto wadogo katika mji huo.

Taratibu mchezo wa soka ukaanza kuwa kivutio kwa mtoto wake mkubwa Hugo Aveiro, kushiriki ligi za vijana pamoja na mdogo wake Ronaldo.

Kutokana na ukata  na  msongo wa mawazo wa wanajeshi wastaafu akiwemo baba yake Ronaldo, walitumia muda mwingi  kunywa pombe kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Ronaldo  akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa akiambatana na baba yake katika vilabu vya pombe na mara kwa mara alinyweshwa pombe kidogo ili aendelee kumsubiri baba yake kabla ya kurejea naye nyumbani.

Mara nyingine kutokana na baba yake kulewa kupindukia, hurejea nyumbani kuwafuata dada na kaka yake ili kuweza kumsaidia.

Pamoja na kulewa kupindukia lakini baba yake Ronaldo hakupenda mwanae aishi kama yeye na alikuwa akimshika begani na kumwambia: “Mwanangu nataka uwe na furaha na upate mafanikio, mimi naishi maisha yangu na wewe uishi maisha yako.”

Ronaldo aliendelea kumlea baba yake hata aliposajiliwa Manchester United, ingawa kuna wakati alikataa mwanae kutumia fedha nyingi kwenye matibabu yake kutokana na kuathirika sana na ulevi, huku akijua ni kupoteza fedha kwa kuwa hali yake ilishakuwa mbaya na muda mfupi baadaye alifariki.

Hivyo, ulevi na kifo cha baba yake ndivyo vilivyomfanya Ronaldo kuanza kuwa mlezi wa familia yake akiwa na umri mdogo.

Mafanikio

Nyota huyo anayepewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na ile ya Ballon D’or, amekuwa na mafanikio makubwa kwenye soka. Ameweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu, mara moja akiwa Man United na mara mbili akiwa Real Madrid pamoja na lile la Euro 2016 na timu yake ya Taifa ya Ureno.

Mafanikio mengine ni mkataba wa muda mrefu na Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike kama ule waliopewa wachezaji wa mpira wa kikapu kama Michael Jordan na sasa LeBron James na mkataba huo wa Ronaldo ukiwa na thamani ya dola milioni 24 kwa mwaka na unatarajiwa kumalizika atakapofikisha umri wa miaka 73.

Pamoja na mkataba huo wa Nike, pia amesaini mkataba mpya na

Real Madrid utakaomalizika mwaka 2021, akiwa na umri wa miaka 36.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -