Wednesday, November 25, 2020

Sakata la kukodishwa Yanga: Heri wenye ‘njaa’ kuliko walioshiba Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU,

TANGU sakata la kukodishwa kwa klabu ya Yanga kuibuka katika Mkutano Mkuu wa  Agosti 6 mwaka huu, misamiati mingi imeibuka ikihusisha klabu hiyo na wanachama wake. Moja ya msamiati au neno ambalo ni maarufu lililokuwepo na ambalo limeibuka kwa kasi ni neno ‘njaa’ likimaanisha watu wasiokuwa na fedha.

Ingawa neno hilo linadhalilisha utu wa watu wanaoitwa, lakini ndiyo linatumika kuwaita wanachama na watu wote wanaounga mkono klabu hiyo kukodishwa kwamba wanaunga mkono kwa sababu ya ‘njaa’ zao kwa kudhani kwamba watu wanaunga mkono wamenunuliwa na mwenyekiti wa klabu hiyo.

Baadhi ya watu wanaopinga Yanga kukodishwa pamoja na watu wa upande mwingine wamekuwa wakiwasema wenzao (wanakubali kukodishwa) kwamba wanakubali kwa sababu ya njaa na wengine wanakwenda mbali zaidi kuwaita wenzao mbumbumbu wasiojua kitu.

Pamoja na maneno na hoja za wale wasiotaka Yanga kukodishwa, lakini tukiangalia msingi wa hoja za pande zote mbili ni wazi kwamba wanaopinga kukodishwa Yanga na kujiita wasio na njaa ndio hao ambao pengine wamekuwa wakinufaika na utajiri mkubwa wa klabu hiyo uliojificha kwa kuwatumia kwa manufaa yao na kuiacha klabu ikiwa masikini isiyojiweza hadi hivi sasa.

Wenye njaa wanaona heri Yanga ikodishwe kwa sababu wanaona kuna manufaa hata kama ni kidogo sana lakini ni heri hicho kidogo kilichowekwa wazi kuliko kikubwa ambacho wamekisubiri kwa miaka mingi bila mafanikio.

Waswahili wanasema ‘heri kenda nenda kuliko kumi nenda urudi’, hivyo ndivyo wale wanaoitwa wenye njaa wanaamini kwani wameahidiwa manufaa ya timu yao miaka mingi, huku kila uongozi ukiingia madarakani kwa ahadi nzuri za kuiendeleza klabu lakini wote wanaondoka wakiiacha klabu masikini wa kutupwa.

Kwanini wanaoitwa wenye njaa wanakataa Yanga ikodishwe? Bila shaka wameona kuna manufaa hasa baada ya kuusoma mkataba wa ukodishwaji uliowekwa hadharani wiki mbili zilizopita kati ya Yanga na Kampuni ya Yanga Yetu Ltd ambayo ndiyo kampuni inayoikodi nembo ya klabu hiyo na timu  ambapo Kampuni ya Yanga Yetu itaitumia nembo ya Yanga SC kibiashara na kisha kuiendesha timu ya Yanga kwa niamba ya klabu ya Yanga SC kwa kipindi cha miaka 10.

‘Wenye njaa’ wanaamini kwamba, kwa hali ya sasa ya uendeshaji wa soka duniani kote ni muhimu sana klabu yao ikabadili mfumo wa uendeshaji, bila hivyo wanaamini kwamba klabu yao haiwezi kusonga mbele na itaendelea kuwa klabu ya soka la ridhaa hasa kwa kutegemea fedha za mifukoni mwa watu kama ambavyo inaonekana hivi sasa ambapo klabu hiyo haiwezi kujiendesha bila ufadhali kwani hata pesa za udhamini hazitoshi kuiendesha klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya wafanyakazi wakiwemo wachezaji na benchi la ufundi.

Kwa sasa malipo ya mishahara kwa wafanyakazi wote klabu ya Yanga ikianzia sekretarieti, wachezaji na benchi la ufundi  inakadiriwa kuwa ni zaidi ya milioni 500 ambazo ni fedha nyingi sana kwa klabu ya Yanga ambayo kwa sasa haina mdhamini na udhamini wa ligi kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na ule wa haki za matangazo wa Sh milioni 100 kwa msimu hazifikii gharama za malipo ya mishahara tu ya mwezi mmoja.

Kwa hali hiyo je, nini linaweza kuwa suluhisho la uendeshaji wa timu ya Yanga? Kuendelea na mfumo huu wa kutegemea ufadhili wa mifuko ya watu au ni muhimu kubadili mfumo? Hoja ya ‘wenye njaa’ inapata mashiko kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa timu hivi sasa hasa kutokana na heshima na hadhi ya Yanga, kwani kwa hali ilivyo kama si ufadhili bado Yanga itarudi nyuma kutegemea mapato ya mlangoni na haitakuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wenye hadhi kwa fedha zao hivyo wataendelea kuwapigia magoti watu wachache jambo ambalo wamelichoka.

Wanaopinga kukodishwa Yanga ambao kimsingi wanajiona hawana njaa pengine wanataka kuendelea na mfumo wa klabu ya Yanga kuwa ombaomba kama ilivyo hivi sasa, wanatamani kuendelea kuiona Yanga ikidhalilika kwa kuwapigia magoti watu wachache, huku wengine wakinufaika na mapato ya milangoni kwani ni ukweli uliowazi kwamba, mapato ya viingilio yameshuka sana siku hizi na hayatoshelezi gharama kubwa za uendeshaji wa timu kama Yanga.

Kwa mujibu wa mkataba wa ukodishwaji, mwekezaji atajenga uwanja na hili ni jukumu lake la kimkataba hivyo ni dhahiri kwamba ‘wenye njaa’ wameona manufaa ya ukodishwaji kwani katika kipindi cha miaka 10 ijayo Yanga itakuwa na uwanja wake na kuepukana na aibu hii ya kufukuzwa Uwanja wa Taifa na aibu kubwa inayowadhalilisha miaka yote ya kukodi viwanja vya kufanyia mazoezi vya shule au vya timu ndogo za mchangani kama Boko Veterani.

Ukiangalia kwa makini, pengine ni suala la utaratibu tu ambalo linatakiwa kufuatwa vizuri, lakini suala zima la ukodishwaji limekaa vizuri na wanaounga mkono wanaweza kuwa wameona unafuu zaidi, kuliko hao walioshiba kwani wao ndio wanaonekana kuwa na ‘njaa’ zaidi ya kutaka kuendelea kuichuma Yanga na kuiacha ikiwa katika lindi kubwa la umasikini katika miaka ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -