Tuesday, October 27, 2020

SALAMBA, MO RASHID WAPEWA MTIHANI SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMAR NA ZAITUNI KIBWANA


KOCHA wa Simba, Patrick Aussems, amepanga kutumia mchezo wa kirafiki kati yao na AFC Leopard kama mtihani kwa wachezaji wake ambao hawapati nafasi katika kikosi cha kwanza akiwamo Adam Salamba na Mo Rashid.

Nyota hao tangu watue Simba wameshindwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba uliopo huku Meddie Kagere na John Bocco wakiwa ndio chaguo la kwanza.

Simba ambao wapo kwenye maandalizi mazito kwenye Uwanja wa Gymkhana kwa ajili ya michezo yao mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara, wamepanga kucheza mchezo huo wa kirafiki Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Aussems anataka kutumia mchezo huo kuwaweka vyema wachezaji wake kufuatia kusimama kwa Ligi Kuu kupisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika wikiendi hii.

Kikosi hicho kina wachezaji sita kwenye timu za Taifa wakijiandaa na michezo ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ambapo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi yupo timu ya Taifa ya Uganda akijiandaa na mchezo dhidi ya Taifa Stars.

Wachezaji wengine wa Simba ambao wako na timu zao za taifa ni kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Meddie Kagere wapo Rwanda wakisubiri mchezo dhidi ya Ivory Coast utakaochezwa mjini Kigali, wakati kipa Aishi Manula yupo Taifa Stars.

Akizungumzia mchezo huo, Aussems alisema anatumia mchezo huo ili kuhakikisha wachezaji hao wanapata namba kwenye kikosi cha kwanza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -