Sunday, October 25, 2020

SAMATTA AAHIDI ‘HAT-TRICK’ NYINGINE

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

 

NA SAADA SALIM


 

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, anayekipiga katika klabu ya KRC Genk, amesema amefurahia kupiga ‘hat-trick’ ya kwanza tangu ametua katika timu hiyo ya Ubelgiji na kuwaahidi mashabiki kuwa atafanya hivyo zaidi.

Samatta amepiga ‘hat-trick’ wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Brondby IF ya Denmark katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Europa League.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Luminus mjini Genk, Samatta amefunga mabao yake katika dakika ya 37, 55 na 70 wakati mabao mengine ya Genk yamefungwa na nyota wa Ubelgiji, Leandro Trossard kwa penalti dakika ya 45 na 90.

Samatta ameliambia BINGWA kwa mtandao kwamba ataendelea kujifua ili kuhakikisha anapiga ‘hat-trick’ nyingine za kumwaga.

“Nimefurahi kufunga ‘hat- trick’ ya kwanza hapa Genk, nina imani nitafunga nyingine nyingi kutokana na kujifua na kufanyia kazi majukumu niliyopewa na benchi la ufundi,” alisema Samatta.

Genk watarudiana na timu hiyo ya Brondby Agosti 30, mwaka huu na wakifanikiwa kuulinda ushindi huo watafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Europa na wanaweza kukutana na Arsenal.

 

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -