Monday, October 26, 2020

SAMATTA ANG’ARA, GENK IKINUKIA MAKUNDI EUROPA LEAGUE

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

 

NA WINFRIDA MTOI

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ameifungia timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji bao kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lech Poznan ya Poland, hivyo kuifanya timu hiyo kunukia katika hatua ya makundi ya Europa League.

Mchezo huo wa marudiano wa raundi ya tatu ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya UEFA ‘Europa League’, ulichezwa kwenye Uwanja wa INEA, mjini Poznan jana usiku.

Samatta alifunga bao hilo dakika ya 19 huku la pili la Genk likifungwa na Leandro Trossard kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45, wakati la Lech Poznan likifungwa na Tomasz Cywka dakika ya 50.

Kwa matokeo hayo, KRC Genk imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 baada ya kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita ambao Samatta pia alifunga bao moja.
Katika hatua inayofuata ya mwisho ya mchujo ili kuingia kwenye makundi, Genk watacheza mechi nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ataingia hatua hiyo.

Mtanzania huyo aliyejiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hivi sasa anawindwa na klabu kadhaa za Ulaya kutokana na mafanikio yake.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -