Tuesday, November 24, 2020

SAMATTA ATAJA KILICHOSHUSHA KIWANGO CHAKE GENK

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, amesema licha ya kuwapo kwa ushindani wa namba katika kikosi cha timu hiyo, lakini kuwa majeruhi kumechangia kutofanya kwake vizuri katika kikosi cha KRC Genk.

Staa huyo wa zamani wa Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa sasa yuko kwenye wakati mgumu baada ya kupoteza nafasi yake ya kuanza katika kikosi cha Genk.

Makali ya mshambuliaji huyo yalianza kupungua baada ya kuumia kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Rapid Wien ya Austria, Septemba 15, mwaka huu ambapo Genk ilishinda mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Laminus Arena.

Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kutoka dakika ya 78, nafasi yake ikichukuliwa na Mgiriki Nikolaos Karelis.

Majeraha hayo yalimweka nje kwa wiki tatu na tangu aliporejea hajafanikiwa kupata nafasi ya kuanza kutokana na  Karelis kufanya vizuri.

“Ninayecheza naye anafanya vizuri, Karelis yuko kwenye fomu nzuri anafunga karibu kila mechi, kwa hiyo anastahili kuanza mechi.

“Binafsi niliathiriwa na majeraha  ambayo yalisababisha kasi yangu kupungua, lakini nitahakikisha najituma zaidi kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi ili niweze kurejea katika kiwango changu cha awali,” alisema straika huyo wa zamani wa Simba na African Lyon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -