Tuesday, November 24, 2020

SAMATTA AWAPA NENO AJIB, MSUVA, MKUDE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUN KIBWANA

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, amewapa neno wachezaji wazawa, akiwamo Ibrahim Ajib, Jonas Mkude na Simon Msuva, kuonyesha kiwango wanapopata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Akizungumza na BINGWA, Samatta alisema mchezaji anayepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio nje anatakiwa kujituma zaidi ili waweze kufuzu.

Samatta amewataka wachezaji  wenzake kutokata tamaa wanapohitaji kwenda kufanya majaribio, kwani wanatakiwa kujituma kwa kiwango cha hali ya juu ili waweze kufuzu.

“Wanapopata nafasi za kutoka basi wazitumie kwa sababu tumeona wachezaji wengi wakitoka, lakini wamekuwa wanarudi nyumbani,” alisema Samatta.

“Unapopata nafasi unatakiwa ulazimishe isiwe rahisi, mtu anakwenda kwenye majaribio halafu anarudi, ikitokea umerudi basi iwe imeshindikana kwa kiasi cha mwisho kabisa,” alisema.

Alisema ikitokea mchezaji ameshindwa basi akirudi nyumbani anapaswa kujipanga kwa ajili ya nafasi nyingine na si kuvunjika moyo kabisa.

“Si lazima uende ukafanikiwe unapofika tu, ukishindwa unakuja kujipanga kwa ajili ya nafasi nyingine na  mwisho wa siku utafanikiwa tu,” alisema.

Wachezaji waliowahi kwenda kufanya majaribio hivi karibuni na kushindwa kupata nafasi ni pamoja na Ajib (Misri), Mkude na Msuva na John Bocco (Afrika Kusini).

Previous articleWAPINZANI WA YANGA HOI
Next articleSIMBA YAITESA YANGA
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -