Wednesday, November 25, 2020

SAMATTA AWAPELEKA ULAYA MSUVA, NDEMLA, KICHUYA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ZAITUNI KIBWANA NA WINNFRIDA MTOI,

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya K.R.C. Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amewapa maujanja nyota wenzake akiwataka kuchangamkia dili za kucheza soka nje na kusema kila mchezaji anayekipiga klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, ana uwezo kutandaza soka la kulipwa Ulaya.

Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, alijiunga juzi na timu hiyo inayojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mazoezi juzi, Samata alisema hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya mtu kutumia na kutambua kipaji kinataka afanye nini.

Alisema anapokuwa Ubelgiji, kuna wakati mawakala wanamuulizia juu ya wachezaji wenye vipaji Tanzania, ambao wanaweza kucheza soka nje na anawatajia, lakini jukumu la kuwatafuta anawaachia wenyewe.

“Siri ya mafanikio kila mtu anayo mwenyewe, naamini wachezaji wote wana vipaji na wanaweza kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Mfano mimi nilifika hapa kwa jitihada zangu mwenyewe, nafasi ilipotokea sikusubiri mtu,” alisema Samatta.

Kuhusu kuporomoka kwa kiwango cha soka kwa Taifa Stars, alisema si suala la kuachiwa baadhi ya watu kulitatua ikiwamo wachezaji, bali ni Watanzania wote  kuungana na kunusuru hali hiyo.

Alisema lawama za kufanya vibaya kwa timu ya Taifa zisiende kwa watu wachache, kinachotakiwa ni kila mmoja kutambua kuwa ana jukumu la kuipandisha Stars kwenye viwango vya ubora.

“Imefika kipindi Watanzania wote kuiangalia timu ya Taifa inafanya nini na inaelekea wapi, ili tuweze kuweka mambo sawa kwa kuwa si suala la mchezaji au mtu mmoja. Haiwezekani wengine wawe wanalia kuona hali hii na wapo wanaocheka,” alisema Samatta.

Samatta aliyeanza kung’ara wakati akiwa na timu ya Mbagala Market, alijiunga na Genk mwanzoni mwa mwaka jana kwa mkataba wa miaka minne akitokea klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo na amekuwa moja ya wachezaji wenye mchango mkubwa katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji hasa kwenye ubachikaji mabao.

Kutokana na mchango huo katika kikosi cha Genk, kumemfanya kuchaguliwa  kwenye kikosi bora cha wiki cha Europa League hivi karibuni, ambacho kilijaa wachezaji lukuki wa timu kubwa Ulaya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -