Wednesday, November 25, 2020

SAMATTA, FARID, MSUVA, AJIB KUONGOZA MAANGAMIZI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

SAADA SALIM NA WINFRIDA MTOI

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inashuka dimbani leo katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku vifaa vinne vikiandaliwa kuongoza maangamizi.

Wachezaji hao waliopewa kazi ya kuhakikisha Botswana wanakufa mapema, ni Mbwana Samatta, Farid Mussa, Simon Msuva na Ibrahim Ajib.

Katika kikosi hicho, wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Samatta na Faridi wanaocheza ligi za nchi mbili tofauti huko Ulaya, wanatarajiwa kuonyesha maujanja yao ya huko walikotoka, yaani Hispania na Ubelgiji.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, alisema hakuna kitakachoharibika kwani amepanga kutumia wachezaji ambao wataiwezesha timu kupata matokeo mazuri kutokana na kutambua kuwa Tanzania ipo katika hali mbaya kiviwango.

Mayanga alisema mchezo huo ni muhimu kwao na wanatakiwa kupata ushindi ukizingatia wana kibarua cha kujiandaa na michuano ya kufuzu  mashindano ya Mataifa Afrika.

“Kikosi nitakachopanga ni cha ushindi, najua wenzetu pia wamekuja wamejiandaa lakini naamini wachezaji niliokuwa nao ni wapambanaji, ambapo nitawatumia wachezaji wote wawili wa  kimataifa katika mechi hii,” alisema Mayanga.

Kwa upande wake, nahodha wa timu hiyo, Samatta, alisema hakuna kingine wanachohitaji zaidi ya ushindi na tayari kocha wa Botswana ameshawamwagia siri kuwa wana vijana wengi wanaotaka kutengeneza majina kupitia mechi hiyo.

“Tumejipanga kupambana na tunajua tunachokihitaji ni kuondoa hii hali iliyopokwa timu ya Taifa hivi sasa, naamini kwa kipindi tulichokuwa pamoja na kocha kimetosha kujiandaa,” alisema Samatta.

Alisema mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na vijana uliofanywa na kocha Mayanga, utasaidia kuifanya Taifa Stars kucheza katika kiwango kikubwa na kuwataka mashabiki kujitokeza uwanjani kwa wingi kuwaunga mkono.

Aidha, kocha wa Botswana, Mwigereza Peter Bulffer, alisema kikosi chake kina vijana wengi na wanautumia mfumo wa kushambulia zaidi hivyo anatarajia mabao katika mchezo huo licha ya kwamba anaijua Tanzania ni timu nzuri.

“Wachezaji wangu wengi ni vijana na wanataka kupitia mchezo huu waonekane na kupata namba za kudumu katika kikosi cha timu ya Taifa kuelekea michuano inayokuja mbele yetu,” alisema.

Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeweka wazi viingilio vya mchezo huo kuwa ni Sh.3000.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -