Friday, October 30, 2020

Samatta kuwafuata Messi, Ronaldo Hispania

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA EZEKIEL TENDWA,

NAHODHA wa Taifa Stars na klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, katikati ya wiki hii atatua Hispania ambako kikosi chake hicho kitaikabili Athletic Club.

Ligi Kuu ya Hispania ndiko wanakokipiga wanasoka wawili wanaoitikisa dunia, Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo.

Kikosi hicho cha Genk kitakuwa wageni wa Wahispania hao mchezo wa marudiano wa Kombe la Uropa League ambapo timu hizo zipo kundi F sambamba na SK Rapid Wien ya nchini Austria na Sassuolo ya nchini Italia.

Katika kundi hilo, kikosi hicho cha akina Samatta kinaongoza kikiwa na pointi sita baada ya kushinda michezo yao miwili kati ya mitatu waliyokwisha kucheza mpaka sasa, wakipoteza mmoja.

SK Rapid Wien wao wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi nne sawa na Sassuolo ambapo kila moja imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja huku Athletic Club wakiburuza mkia wakiwa na pointi tatu.

Katika hatua nyingine kikosi hicho cha akina Samatta mwishoni mwa wiki iliyopita walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Westerlo mchezo wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji na kufikisha pointi 20 katika nafasi ya saba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -