Saturday, October 31, 2020

SAMATTA, MSUVA NDANI YA STARS LEO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...


WINFRIDA MTOI NA MWAMVITA MTANDA

WACHEZAJI wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, wakiwamo Mbwana Samatta na Simon Msuva, wanatarajia kuwasili leo, kujiunga na timu ya Taifa, Taifa Stars.

Taifa Stars ipo kambini jijini Dar es Salaam, ikijiandaa na mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika(Afcon) dhidi ya Uganda itakayochezwa  Septemba 8, mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja  wa Taifa Stars, Danny Msangi, alisema Samatta  anayechezea Genk ya Ubelgiji, atawasili leo Alfajiri na Msuva kutoka  El-Jadida, Morocco anatarajia kufika mchana.

Alisema wachezaji wengine watakaofika leo mchana ni Himid Mao kutoka Petrojet ya Misri,, Shaban Chilunda wa Tenerife ya Hispania na Thomas Ulimwengu  anayechezea El HIlal ya Sudan.

“Wachezaji wote wanaocheza nje ya nchi, watawalisili kesho (leo), ila kila mmoja ana muda wake kutokana na ratiba ya ndege watakazotumia,” alisema Msangi.

Alisema hadi jana wachezaji wakimataifa waliokuwa wamejiunga na kambi ni Rashid Mandawa wa BDF XI ya Botswana na Hassan Kessy anayechezea Nkana FC ya Zambia.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Amunike, amewataka wachezaji wake kufanya kazi kwa bidii.

Alisema, hakuna jambo rahisi kama wao wenyewe hawatafuata kile ambacho anawaelekeza, ni lazima wajitume kuhakikisha kuwa wanakuwa  fiti kujiandaa na mechi hiyo.

“Mwalimu anaweza kufundisha lakini kama mwanafunzi  mawazo yake hayapo darasani basi hatoweza elewa jambo, ndio hata mimi hapa nipo kuwafundisha lazima wafanye kile ninachowaelekeza, bila ya hivyo hatutaweza fanikisha lengo,”alisema Amunike.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -