Monday, August 10, 2020

Samatta na Aston Villa yake wameponea kushuka

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

LONDON, England 

POINTI moja iliitosha Aston Villa ambayo anakipiga nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, kubaki Ligi Kuu Bara baada ya msimu wa 2019/20 kuhitimishwa rasmi jana. 

Samatta ambaye amekuwa chachu kwa timu ya Aston Villa tangu kujiunga nayo Januari mwaka huu akitokea Genk ya Ubelgiji, alicheza dakika 68 kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na kinda, Keinan Davis, katika mchezo dhidi ya West Ham iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1. 

Pointi hiyo moja waliyoipata Aston Villa imewafanya kufikisha pointi 35 ambazo haziwezi kufikiwa na Bournemouth na Watford. 

Shangwe zilitawala katika Uwanja wa Olympic jijini London hususan baada ya Aston Villa kusikia Watford wamefungwa 3-2 na Arsenal huku ushindi wa Bournemouth wa mabao 3-1 dhidi ya Everton bado haukutosha kuwafanya wapande daraja. 

Aston Villa walipata bao dakika ya 84 lililofungwa na Jack Grealish baada ya kupokea pasi ya John McGinn hata hivyo furaha hiyo ilikatishwa ghafla dakika moja kutokana na Andriy Yarmolenko kuisawazishia West Ham. 

Kufuatia Aston Villa kubaki kucheza Ligi Kuu England msimu ujao, timu mbili ambazo zimeungana na Norwich ni Bournemouth na Watford. 

Vita vingine jana vilikuwa kujua timu mbili ambazo zitaungana na mabingwa Liverpool na Manchester City kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. 

Chelsea wakihitaji sare, walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves, mchezo uliochezwa Stamford Bridge.

Mabao yote ambayo yalipatikana kipindi cha kwanza yalifungwa na Mason Mount kwa mkwaju wa adhabu na Oliver Giroud aliyemalizia kiufundi pasi ya Mount. 

Chelsea wanaungana na Manchester United ambao waliwafungwa Leicester City mabao 2-0 mchezo katika mchezo uliochezwa King Power. 

Bruno Fernandez aliwapa Man United bao la kuongoza dakika ya 71 kwa mkwaju wa penalti kabla ya Jesse Lingard aliyeingia kipindi cha pili kutupia ba la ushindi dakika za majeruhi kufutia uzembe kwa kipa, Kasper Schmeichel. 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -