Thursday, October 29, 2020

SAMATTA, WELBECK VITANI ENGLAND

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA AYOUB HINJO

HABARI za straika wa KRC Genk, Mbwana Samatta, kuhitajika na klabu ya Everton ya England, zimezidi kupamba moto baada ya klabu hiyo kumjumuisha Danny Welbeck katika orodha ya washambuliaji wanaowahitaji wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari, mwakani.

Everton wanahaha kuziba pengo la aliyekuwa mshambuliaji wao, Romelu Lukaku, aliyejiunga na Manchester United kwa dau la pauni milioni 75 msimu uliopita.

Tangu kuondoka kwa mkali huyo raia wa Ubelgiji, Everton wameshindwa kupata straika ambaye atakuwa na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu kama ilivyokuwa kwa nyota huyo anayevaa jezi ya Manchester United kwa sasa.

Cenk Tosun ambaye alisajiliwa na Everton msimu uliopita, ameshindwa kuziba pengo hilo mpaka sasa akiwa amefanikiwa kufunga bao moja tu katika michezo iliyochezwa msimu huu.

Everton hawakukata tamaa, dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni kabla ya Ligi Kuu England, waliinasa saini ya winga wa Watford, Richarlson kwa dau la pauni milioni 50.

Richarlson katika michezo sita aliyocheza msimu huu, amefanikiwa kufunga mabao manne huku akionyeshwa kadi nyekundu moja mpaka sasa.

Kufanya vizuri kwa Richarlson kunaifanya timu hiyo kumhamisha nafasi kutoka winga mpaka straika ambako anaonekana kufanya vizuri.

Lakini kocha wa Everton, Marco Silva, anaamini kama timu hiyo itafanya usajili wa straika, itakuwa na nguvu zaidi katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ipo chini ya Richarlson hivi sasa.

Katika orodha ya Silva, kuna majina mawili yamejitokeza kwa nguvu zaidi ambayo ni Samatta wa Genk ya Ubelgiji na Welbeck anayekipiga Arsenal ya England.

Samatta amekuwa kwenye kiwango cha juu tangu kuanza kwa msimu huu, akiwa amefanikiwa kufunga mabao 14 katika michezo 16 ya michuano yote ambayo Genk wameshiriki.

Nahodha huyo wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amefunga mabao saba katika michezo tisa ya Ligi Kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler League, huku mengine saba akifunga kwenye Ligi ya Europa baada ya michezo saba kuchezwa.

Mtanzania huyo mwenye urefu wa futi 5 na inchi 11, anaweza kutengeneza kombinesheni nzuri na Richarlson, huku wachezaji wengine kama Oumar Niasse na Tosun wakisubiri kufunguliwa mlango wa kutokea Januari.

Kwa upande wake, Welbeck amefunga mabao mawili katika michezo nane aliyocheza msimu huu, yaani bao moja katika michezo sita ya Ligi Kuu England na jingine kwenye michezo miwili ya Ligi ya Europa.

Nafasi ya straika huyo wa England inazidi kuwa finyu ndani ya kikosi cha kwanza cha Arsenal kutokana na uwepo wa Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang, walio katika ubora wa hali ya juu.

Samatta yupo katika kilele cha ubora wake hivi sasa, kama watatumia takwimu basi Welbeck itakuwa imekula kwake lakini wakitumia uzoefu wa ligi hiyo itakuwa faida upande kwa straika huyo wa England.

HAWAWEZI KUCHEZA WOTE?

Bila shaka hilo ni sehemu ya maswali ambayo kila mmoja atakuwa akijiuliza baada ya taarifa hiyo kupamba moto katika mitandao ya kijamii.

Kutokana na uwezo wa kila mmoja, wote wanaweza kucheza katika kikosi cha kwanza cha Everton kama watasajiliwa kwenye dirisha dogo la Januari mwakani.

Welbeck ni mchezaji anayeweza kucheza nafasi za mbele zote yaani kama winga wa kushoto au kulia na mshambuliaji wa mwisho au nyuma.

Alifanya hivyo wakati anakipiga Manchester United ambayo ilikuwa na Wayne Rooney, Robin van Persie na Javier Hernandez ‘Chicharito’, mara nyingi akitumika nafasi ya winga wa kushoto au nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

Kwa maana hiyo, Samatta na Welbeck wanaweza kucheza ndani ya kikosi cha Silva huku mmoja wao akitumika nje ya nafasi ya straika kwa ajili ya kumtengenezea mwingine nafasi za mabao.

SAMATTA ATAIWEZA EPL?

Ni sehemu ya maswali muhimu ambayo hivi sasa kila Mtanzania anajiuliza juu ya Samatta kama atafanikiwa kuingia nchini England kwa kasi aliyokuwa nayo sasa.

Mara zote huaminika kusajili mchezaji nje ya Ligi Kuu England, huwa ni kamari ambayo inatakiwa kuwa na subira kama itafanikiwa au itakuwa ndivyo sivyo.

Samatta anafunga mabao nchini Ubelgiji lakini upinzani wa England ni mkubwa zaidi ya huo anaoupata hivi sasa.

Inabidi straika huyo wa Genk kuwa na nguvu, fiti, haraka na mwelewa kutambua ni kipi anatakiwa kukifanya, kwa ufuatiliaji tu Ligi Kuu England inahitaji uwe katika kiwango cha juu kila wikiendi inapofika.

Hivyo vyote Samatta anaweza kuvifanyia kazi kwani wapo wachezaji waliosajiliwa nchini England na kuanza kuonyesha cheche zao bila kusubiri, miongoni mwao wakiwa ni Alexis Sanchez alipojiunga na Arsenal mwaka 2014 au David Silva alipotua Manchester City mwaka 2010.

Lakini pia anaweza kuingia na asifanye vizuri kwa hatua za mwanzoni kabla ya baadaye kubadilika na kuwa mmoja wa wachezaji hatari ndani ya ligi hiyo maarufu duniani kama ilivyotokea kwa wachezaji wengi waliojiunga na EPL.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -