Friday, October 30, 2020

SAMPAOLI AICHIMBIA MKWARA LEICESTER

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

SEVILLE, Hispania

KOCHA wa klabu ya Sevilla, Jorge Sampaoli, amesisitiza kuwa yeye na vijana wake ‘watapigania maisha yao’ katika mchezo wa hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Leicester City, mtanange utakaopigwa Jumatano wiki hii.

Kocha huyo raia wa Argentina alikiongoza kikosi chake kuichapa Eibar mabao 2-0 katika mchezo wa La Liga wikiendi iliyopita, lakini alikiri kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu mno kwa upande wao.

Hata hivyo, Sampaoli ana imani kuwa kikosi chake kitapambana vilivyo kupata ushindi kwenye mchezo huo wa kwanza wa hatua ya mtoano dhidi ya Leicester katika dimba lao la nyumbani la Ramon Sanchez Pizjuan.

Mchezo huo utazikutanisha timu mbili zenye viwango tofauti msimu huu.

Wakati Sevilla ikikamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Hispania (La Liga), mabingwa watetezi Leicester wapo kwenye janga la kushuka daraja katika nafasi ya 17, huku wakiwa na machungu ya kutolewa kwenye michuano ya kuwania Kombe la FA wiki iliyopita.

“Tutapambana na Leicester Jumatano kwa ajili ya maisha yetu na ya klabu. Utakuwa ni mchezo muhimu sana katika historia ya Sevilla.

“Fikra zetu zinatakiwa kuuchukulia huu mchezo kuwa ni wa thamani mno,” alisema Sampaoli.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -