Thursday, December 3, 2020

SANAA INAELEKEA KUWA MWAJIRI MKUU, MIUNDOMBINU IBORESHWE

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

NADHANI utakuwa umewahi kusikia habari za roboti kufanya huduma ya kusambaza vyakula kwenye migahawa  fulani iliyopo katika Bara la Asia hasa nchini China.

Ni mafanikio yanayowafurahisha wanasayansi duniani kote huku kundi kubwa la vijana wenye taaluma ya uhudumu wa hoteli wakilia kwa kuwa vibarua vyao vipo shakani kutwaliwa na roboti hao.

Ni dalili mbaya kwa wote wanaotegemea kupata ajira wakimaliza masomo yao, dunia inakimbia kwa kasi inayopelekea kampuni na mashirika yaliyokuwa yanaajiri wafanyakazi wengi kupunguza idadi ya rasilimali watu kufuatia utundu huo wa wanasayansi.

Mfano mzuri ni hao roboti kutoa huduma kwenye migahawa, utaona kama ilitakiwa kuwe na ajira saba za vijana wahudumu basi ajira sita zitapungua na kubaki ya mtu mmoja anayeziendesha hizo roboti.

Kwenye wakati kama huu tunakutana na vijana waliohitimu ngazi mbalimbali za elimu wakizunguka mtaani na bahasha za kaki kusaka ajira bila mafanikio. Sasa sehemu pekee iliyobaki ambayo inakwenda kutoa ajira kwa wingi ni kwenye sanaa.

Kipaji cha mtu ndiyo ajira yake, elimu ya darasani inaboresha tu kile anachokifanya mtu huyu mwenye kipaji. Ndiyo maana hivi sasa tunaona wimbi kubwa la wasanii wachanga wa muziki na filamu wakijitokeza kwenye mashindano ya kusaka vipaji ili kujaribu bahati zao.

Sanaa mara nyingi inahusisha kipaji kwa maana hiyo mtu anayefanya shughuli za sanaa anakuwa anafanya kazi anayoipenda, hakuna kitu kizuri kama kufanya shughuli unayoipenda hata ukiingia hasara hupati maumivu.

Mwaka 2016 ulikuwa na neena kwa wasanii kwa sababu sanaa ilianza kutambulika kama ajira rasmi. Wasanii wakapewa hadhi sawa na wafanyakazi wengine kwenye ofisi kubwa, hilo ni jambo lililosubiriwa kwa muda mrefu na zaidi tukaletewa waziri ambaye anaifahamu vizuri sanaa.

Mwaka huo huo pia tumeona wasanii wakianza kutengeneza fedha nje ya kazi zao kupitia dili za matangazo, miito ya simu na redio kadhaa zimeanza kuwalipa mirahaba wasanii wa Bongo Fleva pale wanapocheza nyimbo zao.

Hii ni hatua kubwa na muhimu kuwahi kutokea kwenye historia ya sanaa yetu na matarajio ya wasanii ni kuendelea kunufaika na jasho lao. Sasa tumeingia mwaka mpya ambao umebeba matumaini makubwa kwa wasanii maarufu na wale wachanga.

Tunafahamu muziki ulivyotoa ajira nyingi kwa vijana, ni wazi tunaona filamu ilivyogeuka dili kwa watu wengi licha ya miundombinu yake kuwa mibovu.

Wizi wa kazi za sanaa, hadhi ya msanii ili kazi yake iwe kama dhamana ya kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kwa ajiri ya kuboresha kazi zake na mengine mengi bado hayako sawa.

Angalau kwenye sanaa hizo za muziki na filamu wasanii wake hawapo vibaya sana ila ukizitazama sanaa za ubunifu na zile za maonyesho hali ni mbaya na inasikitisha mno ukitazama maisha ya wasanii wale.

Tunawezaje kuweka usawa baina ya msanii wa sanaa moja na nyingine ili siku moja msanii wa muziki awe na maisha sawa na yule mchonga vinyago. Tunawezaje kupunguza wimbi la vijana kukimbilia kwenye muziki na filamu na wakajikita kwenye sanaa za maonyesho na ubunifu?

Hakuna njia zaidi ya kumpa hadhi msanii na kazi yake. Yatafutwe masoko ya uhakika ili wasanii wauze bidhaa zao, biashara ikiwa nzuri msanii huyu atakuwa mtu wa kukopesheka basi anaweza kuingia benki yoyote kwa kufuata taratibu, akapewa mkopo wenye riba nafuu ili aboreshe zaidi kazi zake.

Tukifanikisha hilo basi tunaweza kupunguza kwa kiasi chake tatizo la ajira na sanaa ikawa mwajiri mkuu wa vijana ambao wengi wanakimbilia kwenye filamu na muziki, eti kwa kuwa ukifanikiwa kutoboa basi unatoka haraka kimaisha, itakuwa vyema siku moja wakimbilie kwenye sanaa za ubunifu na zile za jukwaani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -