Friday, October 23, 2020

SANGA MWANZO WA LIGI MGUMU

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

  NA LULU RINGO        |          


Baada ya Klabu ya Singida United kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya timu ya Biashara United ambayo ni wageni kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwenyekiti wa Klabu ya hiyo Festo Sanga amesema timu hiyo imepokea kichapo hicho sababu ni makosa ya kawaida ya kiuchezaji ambayo timu pinzani wameyatumia vyema.

Hata hivyo Sanga amesema mwanzo wa ligi huwa mgumu ndio sababu wapinzani wao wameweza kuwafunga katika uwanja wao wa Namfua huko Singida.

“Ligi inapoanza mambo huwa magumu kuna makosa madogo yaliyopelekea kupoteza mchezo wetu lakini tunaimani tutafanya vizuri kadri ligi inavyoendelea,” alisema Sanga.

Katika hatua nyingine, Sanga ameelezea maendeleo ya mshambuliaji, Habibu Kyombo aliyeko nchini Afrika Kusini kwenye majaribio katika Klabu ya Mamelodi Sundowns kuwa yanaendelea vizuri.

“Tumewasiliana na mchezaji anaendelea vizuri  isipokuwa majaribio anayofanya ni ya ndani hivyo hatujafanikiwa kupata video wala kauli ya viongozi wa timu hiyo lakini mwenyewe anasema anaendelea vizuri,” alisema Mwenyekiti huyo.

Habibu Kyombo alisajiliwa na Singida United kwa kandarasi ya miaka mitatu akitokea Mbao Fc huku akiwa mfungaji bora wa Mashindano ya Azam Sports Federation Cup (FA).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -