Wednesday, October 21, 2020

SANTOS YAITOZA MTIBWA MIL 34/-

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA TIMA SIKILO


 

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema klabu ya Santos ya nchini Afrika Kusini, imetaka kulipwa Dola 15,000 za Kimarekani (shilingi milioni 34 za Kitanzania) kwa awamu kama fidia yao kwa maandalizi waliyofanya kujiandaa kuvaana nao.

Mwaka 2003 Mtibwa ilifungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa miaka mitatu, kutokana na kushindwa kucheza  mchezo wa marudiano dhidi ya Santos kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Mtibwa hivi sasa inajiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kubeba taji la Kombe la FA kwa kuifunga Singida United mabao 3-2, katika mchezo wa fainali uliochezwa Juni 2 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mkurugenzi wa klabu hiyo, Jamal Bayser, alisema pamoja na kuwa wameshailipa faini hiyo, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewataka kulipa tena kwa kuwa wao hawana uthibitisho wa malipo hayo.

Alisema wamezungumza na viongozi wa klabu ya Santos na wamewataka kulipa fedha hiyo mapema, hivyo wao hawana tatizo watapambana ili walipe na kujihakikishia ushiriki wao katika michuano ya kimataifa.

“TFF wametutaka tulipe deni hilo na tumekubali, tumeshazungumza na viongozi wa klabu ya Santos na wanahitaji kulipwa Dola 15, 000 za Kimarekani ambazo tumeomba tuwalipe kwa awamu tatu,” alisema Bayser.

Hata hivyo, aliongeza kuwa wanatarajia kuanza kulipa kuanzia mwezi huu na kumaliza Desemba mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -