Thursday, November 26, 2020

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na MWANDISHI WETU, MWANZA

BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha shabiki kindakindaki wa Simba, Shaaban Jumanne ‘Balwe’ wa jijini Mwanza, aliyefariki baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Taarifa za kifo cha Balwe, zimethibitishwa na Katibu wa Matawi ya Simba Mkoa wa Mwanza, Filbert Kabago ambaye alisema marehemu alifikwa na umauti akiwa katika kibandaumiza kwa Mwalimu Said, wakati akitazama mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu hizo za Kariakoo, Dar es Salaam, zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Kabago alisema kuwa mara baada ya Yanga kupata penalti baada ya winga wao, Tuisila Kisinda kufanyiww madhambi eneo la hatari, marehemu alianza kujisikia vibaya kwa mwili kuishiwa nguvu na akajikongoja kutoka nje kupata hewa, lakini hali ikazidi kuwa mbaya na kufikwa na umauti.

Alisema marehemu alianza kutazama mchezo huo katika kibandaumiza kinachoitwa Vidumu kabla ya kuelekea kwa Mwalimu Said ambako andiko umauti ulikomkuta.

Marehemu ambaye aliwakuwa kuwa kipa makini enzi, amezikwa jana Jumapili huko Mwanza na na mziko yake kuhudhuriwa na mashabiki na wanachama kibao wa Simba na hata wale wa Yanga wa jijini humo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -