Tuesday, November 24, 2020

SASA LWANDAMINA ASHINDWE MWENYEWE YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA EZEKIEL TENDWA

YANGA wamelifanyia mabadiliko makubwa benchi lao la ufundi, hasa baada ya kumleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina, huku Hans van der Pluijm akipewa majukumu mengine ya kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Sababu kubwa ya viongozi wa Yanga kulifanyia mabadiliko benchi lao hilo ni kutokana na kiu waliyonayo ya kutaka kuiona timu hiyo kongwe hapa nchini ikipiga hatua kubwa, hasa katika michuano ya kimataifa.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanafahamu kuwa hawana historia ya kufanya vizuri linapokuja suala la michuano ya kimataifa, ndiyo maana mabosi wao wameamua kumwaga fedha kwa kadri wanavyoweza kuimarisha benchi la ufundi ili kupata matokeo mazuri msimu huu.

Katika michuano hiyo ya kimataifa, Yanga watashiriki Klabu Bingwa Afrika mwakani na wanajua kuwa watakutana na timu kubwa zenye uzoefu usio na shaka, ndiyo maana nao wakaamua kufanya kweli kwenye suala la benchi la ufundi.

Mabosi wa Yanga wamechungulia uwezo wa Lwandamina, hasa alipokuwa akiifundisha Zesco ya Zambia, wakagundua kuwa anaweza kuwafikisha mbali akishirikiana na mkurugenzi wa ufundi ambaye ni Pluijm, ndipo wakaamua kumvuta.

Wakati makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga anamtambulisha Lwandamina kama Kocha Mkuu na Pluijm kama Mkurugenzi wa Ufundi, alisema wao kama viongozi watampa kila kitu anachokitaka na ushirikiano wa hali ya juu, lengo likiwa ni kuiona timu ikiongozwa kisasa.

Maana kubwa ya maneno ya Sanga ni kwamba, viongozi hawatathubutu kuingilia majukumu ya kocha na kile ambacho atakihitaji watampatia bila kikwazo chochote, hiyo ikimaanisha kuwa, sasa Lwandamina ashindwe mwenyewe.

Nakumbuka wakati Sanga anamaliza kumtambulisha Lwandamina, maneno yake ya mwisho alisema “sasa jamani hawa wawili (Lwandamina na Pluijm) wanakwenda kukaa meza moja na kuangalia namna ya kuijenga Yanga”.

Ni jambo zuri sana kocha anapopewa uhuru wa kutosha na kuepukana na ile kasumba ya baadhi ya viongozi kuingilia majukumu ya benchi la ufundi. ikiwamo kumpangia kocha kikosi atakachokipanga, hali ambayo ilikuwa ikiwapata baadhi ya makocha waliopita, hasa hizi timu mbili za Simba na Yanga.

Kazi kubwa aliyonayo Lwandamina kwa sasa ni kuhakikisha yale mafanikio aliyoyapata Pluijm anayaendeleza, kwani vinginevyo wana Yanga hawatamuelewa, ikizingatiwa kuwa uongozi umeahidi kumpatia kila kitu.

Katika suala la usajili, Lwandamina amepewa vigo mpana wa kusajili mchezaji yeyote anayemtaka, kwani suala la fedha siyo tatizo, ndiyo maana tumeanza kuona sura mpya kwa wanajangwani hao, akiwamo kiungo mkata umeme, Justine Zulu.

Kikubwa ambacho Lwandamina anatakiwa kukifanya ni kuhakikisha Yanga wanatetea ubingwa wao na pia kupiga hatua kubwa katika michuano hiyo ya kimataifa, hasa ikizingatiwa kuwa ndicho alichoitiwa.

Msimu uliopita Yanga walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku wakifika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika na sasa wamemleta Lwandamina, lengo likiwa ni kupiga hatua nyingine mbele zaidi.

Viongozi pamoja na mashabiki hawataki tena kuiona timu yao ikiishia hatua za awali michuano hiyo ya kimataifa, wanataka kuiona timu ikishinda, lakini pia ikicheza soka la kuvutia, ili kudhihirisha kuwa wao ni moja ya timu zenye heshima katika bara hili la Afrika.

Jambo la kufurahisha ni kwamba, katika utambulisho wake, Lwandamina alisema anahusudu sana soka linalochezwa na Barcelona ya nchini Hispania, hiyo ikimaanisha kuwa, ndilo soka ambalo tunatarajia kuliona kwa Yanga.

Naamini Lwandamina atapewa kila kitu, ikiwamo kuipeleka timu kambi sehemu yoyote atakayotaka yeye, kwani katika misimu ya hivi karibuni tulishuhudia Pluijm akiipeleka Uturuki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -