Tuesday, December 1, 2020

Sasa Ronaldo atoka na mtoto wa wakala wake

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MADRID, Hispania

MIONGONI mwa mastaa ambao wanasifika kwa tabia zao za kujiachia na warembo ni Cristiano Ronaldo.

Ni ngumu kuliweka kando jina lake unapotaja orodha ya wanasoka wanaopenda walimbwende.

Utamtaja Ashley Cole, Mario Balotelli, Clint Dempsey, Samir Nasri, Frank Ribery, lakini mwishowe huwezi kumsahau Ronaldo.

Kwa nyakati tofauti, winga huyo wa kimataifa wa Ureno aliwahi kutoka kimapenzi na warembo wengi tu, wakiwemo

Paris Hilton, Irina Shayk, Merche Romero, Kim Kardashian na Nuria Bermudez.

Mbali na wasichana hao, pia nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno hakuwaacha warembo, Niki Ghazian na Jordana Jardel.

Mwaka jana, aliamua kumaliza kabisa kwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na binti wa wakala wake wa siku nyingi, Jorge Mendes.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 25, anaitwa Marisa Mendez.

Hayakuwa matarajio ya wengi kumuona Ronaldo akitolewa udenda na msichana huyo hasa kutokana na uswahiba mkubwa kati yake na wakala Mendez.

Ni mara ngapi umewahi kusikia au kuona mtoto wa bosi akitoka kimapenzi na mfanyakazi wao?

Ingawa inaonekana ni ngumu kwa kiasi fulani, kwa Ronaldo ilikuwa kama kusukuma mlevi.

Staa huyo wa Real Madrid, akavunja ukimya na kuamua kukabidhi moyo wake kwa mwanadada huyo.

Ronaldo na Marisa mwenye umri wa miaka 25 walianza kuhusishwa na uhusiano wa kimapenzi mwaka uliopita.

Hata hivyo, mara kadhaa wawili hao walikanusha vikali taarifa kuwa wako kwenye mahaba mazito.

Imeripotiwa kuwa Ronaldo amekolezwa na penzi la mlimbwende huyo kiasi cha kumwajiri kuwa mtaalamu wake wa masuala ya kijamii.

Taarifa za Marisa ‘kupenzika’ na Ronaldo zimemfanya mlimbwende huyo kujiongezea wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.

Inasemekana mwanadada huyo ana wafuasi wanaotajwa kufikia 82,100 ambao mara nyingi wamekuwa wakisifia urembo wake.

Kutokana na uamuzi huo wa Ronaldo, ni wazi sasa hakuna kificho juu ya ukaribu wao wa ‘kimalavidavi’.

Miongoni mwa majukumu mapya ya kikazi atakayokuwa nayo Marisa ni kushughulikia mawasiliano ya Ronaldo katika mitandao ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mwanamichezo wa kwanza kufikisha wafuasi milioni 200 katika akaunti zake za mitandao ya Facebook na Twitter.

Mpaka sasa mwanasoka huyo ana wafuasi wapatao milioni 244 katika akaunti zake za mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter.

Hivyo, Marisa atakuwa na kibarua cha kusimamia akaunti hizo za mitandao ya kijamii.

Ni miezi michache imepita tangu Marisa alipohitimu masomo yake ya masuala ya masoko.

Baada ya baba yake kuingiza fedha nyingi kutokana na uhamisho wa Ronaldo kutoka Man United kwenda Madrid, sasa ni zamu ya Marisa kuvuna mpunga mrefu kutoka kwa Mreno huyo huku ikiwa ni nafasi nzuri ya kuendelea na uhusiano wao wa kimapenzi.

Akimzungumzia wakala Mendes, Ronaldo alisema bosi huyo ni zaidi ya baba au kaka yake.

Kipindi fulani wakati Mendez alipokuwa akioa, Ronaldo alimnunulia wakala huyo kisiwa nchini Ugiriki ikiwa ni zawadi yake ya ndoa.

Kuna taarifa zinazodai kuwa mbali na Marisa, Ronaldo anachepuka na mwanamitindo Desire Cordero.

Kwa wafuatiliaji wa maisha ya staa huyo, wanajua kuwa Cordero ni mshindi wa zamani wa taji la urembo la Hispania ‘Miss Hispania’.

Taarifa za Ronaldo kuwa na ukaribu na Cordero zilianza kuvuma miezi kadhaa iliyopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -