Wednesday, November 25, 2020

SAVIO MKIMTUMIA VIZURI MAIGE MTATETEA TAJI LENU LA RBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SHARIFA MMASI

KWA wanaofuatilia Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, bila shaka watakuwa wameshuhudia kiwango cha nyota wa Savio, Sylvian Yunzu ‘Maige’, ambaye anastahili hata kuitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo huo.

Maige amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wanaofuatilia ligi hiyo inayoendelea kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, kutokana na kuonekana kuwafunika nyota wengine wa mchezo huo.

Nyota huyo ameonekana kuwafunika wachezaji wengine wa mchezo huo wakiwamo wakongwe kama Franklin Simkoko, Himid Choka wote wa JKT na wengine wengi, lakini pia katika timu yake anaendelea kuwafunika wachezaji waliowahi kutamba miaka ya nyuma akiwamo Muhammed Yusuph ambaye pia ni kocha wa timu ya DB Lioness, Ally Mnyamani, George Tarimo na wengineo.

 

Savio wana nafasi nzuri ya kutetea taji lao kama wataendelea kumtumia vizuri mchezaji huyo kipindi hiki ambacho mzunguko wa kwanza unaelekea ukingoni.

Si hivyo tu, pia Savio wakimtumia vema kwenye mzunguko wa pili uliopangwa kutimua vumbi Mei mosi mwaka huu, atawasaidia kuweka rekodi ya kuchukuwa taji la ubingwa na kutopoteza mchezo hata mmoja msimu mzima wa RBA.

Kasi ya Maige na uwezo wake wa kukaba bila ya kufanya makosa ya mara kwa mara yamekuwa na mchango mkubwa kwa Savio katika mbio zao za kutetea ubingwa wao huo wa RBA.

Kwa sasa nyota huyo wa Savio anaongoza kwa kufunga vikapu vingi kwenye ligi hiyo ya RBA, ambapo amefanikiwa kutupia vikapu 195, akifuatiwa na mchezaji wa Ukonga Kings, Ally Hashim, mwenye vikapu 186 na Yassin Choma wa Kurasini Hits anashika nafasi ya tatu kwa kuambulia vikapu 181.

Ukiachana na vikapu hivyo vya kawaida, Maige anaongoza kwa kufunga nje ya D, ambapo ametupia jumla ya vikapu 43 akiwa kwenye eneo hilo, huku anayemfuatia Erick Lugola wa Oilers akiwa na mitupo 23 nje ya eneo hilo la D.

Vikapu hivyo vya Maige, vimeifanya Savio kuongoza msimamo wa ligi hiyo, wakiwa na jumla ya pointi 22 baada ya kucheza michezo 11.

Moja ya kitu ambacho Savio hawapaswi kufanya kwa sasa ni kutomweka benchi mchezaji wao huyo, ambaye tangu ligi hiyo ianze ameonyesha nidhamu ya juu ya uchezaji kwani hajawahi kutolewa kwenye mchezo wowote kwa kucheza faulo zaidi ya nne, hivyo kuwa naye kwenye mechi unakuwa na uhakika wa ulinzi na mtu wa kumaliza naye mechi nzima.

Savio wanamhitaji sana Maige kwani urefu na umakini wake wakati wa kufunga ni kitu ambacho kitatoa mchango mkubwa kwa timu hiyo ili kuendelea kujikita kileleni na kuweza kutetea taji lao.

Pamoja na urefu na uwezo wake wa kufunga kila anapopata mpira mbele ya goli, pia uzoefu wa Miage alioupata nchini Uganda alipochezea timu za Worries na Our Savio, ni kitu kingine ambacho Savio wanakihitaji kwenye harakati zao hizo za kutetea taji lao.

Uwepo wake uwanjani nao unaisaidia sana Savio, kutokana na kutishia timu nyingi ambazo mara kadhaa zimekuwa zikimpigia hesabu namna ya kumkaba yeye, huku wachezaji wengine wa Savio wakiendelea kuisaidia timu.

Hivyo Savio kama watamtumia vizuri mchezaji huyo bila ya shaka watapata ushindi kwenye mechi nyingi na kutetea taji lao la RBA.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -