Sunday, October 25, 2020

SERENGETI BOYS IANDALIWE VYEMA TUSITIE AIBU

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA

WIKI hii Watanzania walikuwa kwenye furaha kubwa baada ya timu yao ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kurejeshwa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo.

Tanzania imerejeshwa kwenye michuano hiyo baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Kongo Brazzaville iliyomtumia mchezaji aliyezidi umri.

Kijeba, Langa Lesse Bercy, aliyedaiwa kucheza Ligi ya Congo alifunga bao pekee lililoivusha timu hiyo ambayo katika mchezo wa kwanza ilishindwa mabao 3-2, lakini ikaiondoa Serengeti kwa bao 1-0 dakika za majeruhi nyumbani na kuipeleka Congo fainali za Afrcon U-17 zilizopagwa kufanyika Antananarivo, Madagascar kabla ya kuhamishwa Gabon.

Kutokana na kuondolewa kwa Serengeti Boys, Shirikisho la Soka Tanzania, TFF iliwasilisha malalamiko, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambao walikitaka Chama cha soka Congo, (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji huyo Misri kwa ajili ya vipimo vya MRI ili kuthibitisha umri wake.

Congo walitakiwa kumpeleka mchezaji huyo makao makuu ya CAF mjini Cairo, Mirsi, kwa vipimo lakini mara mbili walishindwa kufanya hivyo na kuipa nafasi Tanzania kusonga mbele.

Serengeti sasa wamepangwa kundi B pamoja na Angola, Mali na Niger katika fainali za vijana zitakazoanza Aprili 2 mwaka huu nchini Gabon.

Ni wazi kabisa kuwa mbio za vijana hao wa kocha Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’, kwa kuangalia ‘performance’ ya kikosi cha sasa cha Serengeti wameonyesha kuwa wanaweza kufanya makubwa.

Ninaamini matunda mazuri ya vijana wetu waliyoyapata wana nafasi nzuri ya kufika mbali.

Hata kama ni kweli Serengeti Boys hii haiwezi kufanana hata chembe na timu ile ya mwaka 2004-2005 iliyoundwa na kina Athuman Idd ‘Chuji’, Nizar Khalifan, Nurdin Bakar, Juma Jabu Jumanne Ramadhani ‘J4’ Godfrey Mmasa, Julius Mrope na wengineo chini ya makocha Abdallah Kibadeni na msaidizi wake marehemu Sylvester Marsh.

Baada ya kupata nafasi hiyo ni wazi kwamba muda uliopo ni mchache sana kufanya maandalizi, hivyo ni vyema sasa TFF kwa kushirikiana na wadau wakafanya jitihada za makusudi katika kuhakikisha timu hiyo inaweka kambi ya uhakika.

Mara nyingi soka letu limeshindwa kupiga hatua kutokana na sababu kadhaa ikiwamo ya maandalizi dhaifu ya timu za taifa, lakini kwa TFF na Serikali nawapongeza kwa kudhamini safari ya timu hii kuweka kambi nchi mbalimbali kama vile Madagasca na Korea.

Kwa kile kilichoonyeshwa na vijana wetu tuna hakika sasa kazi kubwa ni kuhakikisha timu inaandaliwa vizuri kwa ajili ya fainali hizo.

TFF kama wasimamizi wakuu wana dhamana ya kuhakikisha vijana wetu wanaendelea kupewa kila kinachowezekana kama sehemu ya maandalizi ya michuao hiyo.

Kama wadau wa michezo, tunaamini kuwa vijana wetu wataendelea kuandaliwa vizuri na kupata mechi nyingi za majaribio, wanaweza kuwa alama ya ukombozi wa soka la Tanzania katika ngazi ya kimataifa.

Uwezo walioonyesha vijana wetu umetoa tafsiri ya uwapo wa vipaji vya soka nchini.

Kama kweli tunapenda kuiona Serengeti Boys ikiendelea kufanya vizuri ni lazima kuwekeza nguvu ya pamoja.

Ifike mahali wadau wa michezo tujione tuna deni kubwa la kuikomboa Tanzania katika medali ya kimataifa na hili litawezekana kwa kuunganisha nguvu.

Kadhalika, hii ni fursa pia kwetu kuwakumbusha vijana wetu kubaki kwenye maadili ya kimichezo na kuepuka aina yoyote ya vitendo vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Hivyo basi, wakati tukifurahishwa na matunda ya vijana wetu, wachezaji wenyewe wana jukumu la kulinda vipaji vyao kuzingatia programu za mazoezi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -