Sunday, October 25, 2020

SERENGETI BOYS KUWAWASHIA MOTO UGANDA LEO?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA WINFRIDA MTOI


ULE moto uliowashwa na vijana wa timu ya Taifa wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, unatarajia kuendelea leo Uwanja wa Taifa, watakapokutana na Uganda, katika mchezo wa nusu fainali wa michuano ya CECAFA ya kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCON-U17) itakayofanyika nchini mwakani.

Serengeti inakutana na Uganda waliompiga Djibouti kipigo cha mbwa koko cha mabao 8-0 juzi, hali iliyowafanya wamalize katika nafasi ya pili kwenye kundi B na pointi sita baada kushinda mechi mbili na kupoteza moja.

Lakini kwa upande wao, vijana hao wa JPM yaani Serengeti, wamemshinda mechi zote tatu za hatua ya makundi kwa kuifunga Burundi 2-1, Sudan 5-0 na Rwanda 4-0 zilizokuwa kundi A na kujikusanyia pointi tisa, ikifuatiwa na Rwanda iliyojikusanyia pointi sita.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Oscar Milambo, alisema wamejipanga kukabiliana na timu hiyo kwa sababu ni miongoni mwa vikosi vilivyofunga mabao mengi.

Alisema anaamini vijana wake wataendelea kuwapa raha Watanzania kutokana na ujasiri waliokuwa nao na hamu ya kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.

“Tumejiandaa vema, tunatarajia mchezo utakuwa mgumu, kwani Uganda katika mechi zake za nyuma ameshinda mabao mengi,” alisema.

Katika mchezo mwingine Rwanda watakutana na vinara wa kundi B, Ethiopia; mechi zote zikipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -