Saturday, November 28, 2020

SERENGETI BOYS: SAFARI YA MADAGASCAR INAWEZEKANA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY,

TIMU ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’, imekula ng’ombe mzima na kubakisha mkia kufuzu fainali za Kombe la Afrika kwa vijana, zilizopangwa kufanyika mwakani nchini Madagascar.

Serengeti Boys imebaki na mtihani mmoja kufuzu fainali hizo, ambao kesho watacheza  na vijana wenzao wa  Congo Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Ni mechi muhimu kwa Serengeti Boys kushinda kwenye uwanja wake wa nyumbani, kwani  itakuwa imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu.

Ushindi kwa Serengeti Boys utakuwa umewaweka katika nafasi nzuri ya kusongo mbele katika mechi ya marudiano itakayochezwa nchini Brazzaville.

Endapo Serengeti Boys itafanikiwa kuitoa Congo-Brazzaville, itafanikiwa kuingia katika fainali za mashindano hayo zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Madagascar.

Serengeti Boys ina kila sababu ya kuibuka na ushindi kutokana na maandalizi ambayo wamefanya, lakini watacheza mbele ya mashabiki wao ambao watashangilia kwa ajili ya kuwapa hamasa ya kushinda.

Kutokana na uwezo ulioonyeshwa na Serengeti Boys katika mechi za awali, kufuzu katika michuano inawezekana, iwapo kesho watafanya kile walichokifanya kwa wenzao.

Safari ya Serengeti Boys kwenda Madagascar ilianzia kwenye Uwanja wa Taifa, jijini, pale ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Shelisheli, kisha iliibuka na ushindi wa mabao 9-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa ugenini.

Baadaye walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na wenzao wa Afrika Kusini  ugenini, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0  kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinaingia uwanjani kikitoka kuweka kambi ya siku 10 Shelisheli, ilikopata nafasi ya kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Northern Dynamo na kushinda bao 1-0.

BINGWA imepata nafasi ya kuzungumza na kocha wa timu hiyo, Bakari Shime na msaidizi wake, ambapo wote wanasema kuwa lengo lao ni kuona timu inacheza fainali za mashindano hayo.

Bakari anasema kambi waliyopiga  Shelisheli na mechi ya kirafiki waliyocheza imeweza kumsaidia kufanya marekebisho ya makosa aliyoyaona katika mechi dhidi ya Afrika Kusini, licha ya kushinda 2-0.

“Hadi sasa kikosi changu hakina majeruhi, kambi tuliyoweka imeweza kuongeza uzoefu mkubwa wa kuja kupambana na vijana wa Congo, kwani nimeweza kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wetu na Afrika Kusini.”

Shime haachi kulishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kuhakikisha timu inajiandaa kikamilifu.

Anasema, licha ya kwamba TFF haiko vizuri kiuchumi, lakini imeweza kupigana ili kuhakikisha Serengeti inafanya vizuri katika michuano hiyo.

“Congo Brazzaville siyo timu ya kuibeza, ukizingatia pia historia inaonyesha mara nyingi tumekuwa tukipoteza mbele yao, lakini kwa maandalizi tuliyofanya tuna nafasi kubwa ya kucheza fainali.

“Kikubwa ni wachezaji kutimiza majukumu yao kwa kupata ushindi nyumbani wa idadi kubwa ya mabao ambayo yatakuwa na faida kwetu katika mechi ya marudiano wiki mbili zijazo,” anasema.

Sebastian Nkoma, ambaye ni kocha msaidizi wa timu hiyo, anasema: “Hii siyo timu ya watu fulani, ni timu ya taifa, hivyo kila Mtanzania anahitajika kutoa mchango wa hali na mali, ili tuweze kufikia mafanikio ambayo kila mmoja anatamani kuona siku moja timu ya taifa ya soka imefika.”

Nahodha wa kikosi hicho, Issa Abdull,  anasema: “Nina imani tuna uwezo mzuri wa kupambana na kila aliye mbele yetu, kutokana na maandalizi tuliyofanya, hususan katika mashindano ya kimataifa ya kirafiki tuliyocheza.

“Watanzania watuamini tunaweza kuifikisha timu hatua ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana na kazi hiyo tunaitimiza Jumapili kwa kuwafunga wapinzani wetu idadi kubwa ya mabao.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -