Tuesday, October 27, 2020

SERENGETI BOYS  TUPENI RAHA WATANZANIA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

TIMU  ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo inatarajiwa kucheza na Rwanda katika mchezo wa Kundi A, wa kuwania kufuzu fainali za vijana Afrika (Afcon U-17), utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dares Salaam.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limeipa Tanzania  kuandaa michuano hiyo  kwa sababu  itakuwa wenyeji wa fainali Afcon kwa vijana zitafanyika mwakani.

Tayari Serengeti Boys imecheza michezo miwili dhidi ya Burundi na kushinda mabao 2-1, kabla ya kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sudan.

Tunaamini kwamba Serengeti Boys wataendelea kuwapa raha Watanzania kwa kupata ushindi mwingine dhidi ya Rwanda ili waweze kuongoza katika kundi lao.

Ushindi kwa Serengeti Boys dhidi ya Rwanda utendelea kuwapa matumaini Watanzania kuwa wanaweza kukabiliana na timu yoyote itakayofuzu fainali hizo.

Pamoja na Tanzania  tayari imekata tiketi ya moja kwa moja kushiriki fainali  hizo  kwa kigezo cha kuwa mwenyeji, lakini Watanzania wanahitaji kuona kiwango zaidi  kwa Serengeti Boys.

BINGWA tunasema kwamba michuano ya Caf-Cecafa ni muhimu kwa Serengeti Boys kujiandaa na fainali hizo ili kuweza kuchukua ubingwa wa Afrika kwa vijana.

Tunasema kwamba michuano hiyo, itatoa taswira kamili maandalizi ya Serengeti Boys, kabla ya kupigwa fainali katika ardhi yetu.

Tunaamini kwamba, baada ya michuano ya Caf-Cecafa, Serengeti Boys  watakuwa  wameongeza uzoefu mkubwa  wa kucheza michezo mingi ya kimataifa, baada ya ile iliyofanyika  Mei mwaka huu,  Burundi na kutwaa ubingwa.

BINGWA tunasema kwamba michuano  ya Caf-Cecafa ina faida kubwa, hasa kwa benchi la ufundi wa Serengeti Boys kuweza kubaini mafungufu na kuyafanyika kazi kwa haraka kabla ya kuanza kwa Afcon U-17.

Tunaamini kwa matayarisho yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na benchi la ufundi, yataendelea kujenga kikosi bora cha Serengeti Boys na kuweza kufanya makubwa.

Tunaitakia kila la heri Serengeti Boys.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -