Saturday, November 28, 2020

SERENGETI, GHANA SOKA MARIDADI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

TIMU ya soka ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, jana imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Black Starlets ya Ghana kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwenye mchezo huo, Serengeti Boys ilicheza soka maridadi ambapo safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Abdallah Rashid, iliweza kushambulia lango la wapinzani wao mara kwa mara lakini walizidiwa mbinu na vijana hao wa Ghana.

Serengeti Boys walianza kufungwa kwenye dakika ya 22 na Salley Ibrahim wa Ghana baada ya kumalizia pasi ndefu ya Levesh Gabriel. Ghana wanaonolewa na Samwel Kwasi, walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 73 kupitia kwa Arko Mensah, aliyepiga mpira wa faulo baada ya mchezaji wao, Sulley Ibrahim, kuchezewa rafu. Baada ya mabao hayo Serengeti Boys haikuvunjika moyo na kupambana na kufanikiwa kupata penalti kwenye dakika ya 87 iliyoamuriwa ipigwe na mwamuzi Elly Sasii, baada ya mchezaji wa Ghana kuunawa mpira.

Bao hilo la penalti lilifungwa na Assad Juma ambapo ndani ya dakika za nyongeza, Muhsin Malima, aliifungia Serengeti Boys bao la pili kwa kumalizia krosi ya Ally Msengi.

Licha ya kuanza kufungwa Serengeti Boys  ilipambana kwenye kipindi chote cha kwanza na cha pili ambapo dakika ya 28 na 60 straika Yohana Mkomola nusura awanyanyue Watanzania kama angekuwa makini kumalizia krosi ya Nickson Job.

Kabla ya mchezo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, aliwakabidhi rasmi bendera ya Taifa timu hiyo inayoondoka leo nchini kwenda Morocco kwa ajili ya kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na mashindano hayo. “Nimewakabidhi bendera, mmebeba matumaini ya Watanzania wengi, tunahitaji taji hapa wekeni uzalendo mbele mpigane kwa ajili ya Watanzania,” alisema Dk. Mwakyembe.

Kikosi hicho kinatarajia kusafiri leo kwenda nchini Morocco kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.

Ikiwa huko itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji Morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au Misri. Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi, mwaka huu na timu itasafiri hadi Cameroon.

Ikiwa Cameroon, Serengeti Boys itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na 6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, kwenda Gabon ambako imepangwa Kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.

Serengeti: Ally Msengi, Ramadhani Kabwili, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ally Ng’anzi, Assad Juma, Shaban Zubery, Yohana Mkomola, Kelvin Naftar na Abdallah Rashid/Muhsin Malima

Ghana: Ayiah Eric, Ibrahim Danlad, Yakubu Najeed/Iddriss Mohammed, Alhassan Rashid, Osman Faisal, Yusif Abdulrazak, Owusu Terry/Arko Mensah, Antwi Kwame/Antah Isaac, Levesh Gabriel, Sulley Ibrahim, Toku Emmanuel.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -