Sunday, January 17, 2021

Serengeti yatwishwa zigo la Stars 2021

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA SALMA MPELI

BAADA ya kushindwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, kikosi cha timu ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ sasa kinaandaliwa kwa ajili kuchukua majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinzi, alisema lengo la ofisi yake ni kuhakikisha wachezaji wa timu hiyo wanaendelea kupikwa hadi mwaka 2021 ambapo wataunda kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki fainali za mataifa ya Afrika.

“Baada ya mechi ya jana (juzi), vijana walilia sana, imewaumiza kupoteza mchezo huo, lakini ndiyo soka hata hivyo tutakula nao chakula cha mchana Jumatano na kikubwa tutajulisha kwamba wao sasa ndiyo Ngorongoro Hereoes ya 2019 na taratibu tutajenga Taifa Stars ya 2021 kwa kuwashirikisha kwa karibu vijana hawa.

“Timu hiyo inatarajiwa kujerea leo saa 3 usiku kwa ndege ya Rwanda, ambapo Jumatano watakutana na viongozi kwa ajili ya kuzungumza nao matarajio yao na kikubwa viongozi kukaa karibu na kuwapatia mechi hasa za kimataifa kwa ajili ya kuwaandaa,” alisema Malinzi.

Serengeti juzi ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Congo kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Debat mjini Brazzaville katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo.

Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inatolewa kwa bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3, kufuatia kushinda 3-2 katika mechi ya kwanza wiki mbili zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -