Tuesday, October 20, 2020

Serge Aurier amuokoa mchezaji aliyemeza ulimi

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Bouake, Ivory Coast

BEKI wa Ivory Coast, Serge Aurier, ameokoa maisha ya kiungo wa Mali, Moussa Doumbia, aliyekuwa amemeza ulimi.

Mchezaji huyo wa klabu ya Paris Saint-Germain, Aurier, ambaye baadaye alishutumiwa kwa jinsi alivyoshangilia bao, alimuwahi Doumbia na kuuvuta ulimi na kumlaza vizuri baada ya kuangukia uso.

Doumbia aliangukia uso baada ya kugongana na beki wa Sunderland, Lamine Kone.

Kocha wa Mali, Mfaransa Alain Giresse, amemshukuru Aurier kwa kujifikirisha kwa haraka na kumsaidia mchezaji wake wakati wa mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 kwa timu za Afrika mjini Ivory Coast mwishoni mwa wiki iliyopita.

Giresse alikiambia kituo cha redio cha Ufaransa cha RMC: “Serge Aurier pamoja na wachezaji wetu walimgeuza Doumbia na kumlaza chali na kutumia mkono wake kuuvuta ulimi wakati anakaribia kufa.”

“Kilikuwa kitendo cha kipekee sana kutoka kwa Aurier. Nilizungumza naye baada ya mechi kumalizika na kumshukuru kwa kujiongeza.”

Naye Kocha wa Mali, Fousseni Diawara, alisema: “Doumbia alianguka na kumeza ulimi wake na Serge alikuwa mtu wa kwanza kufika na kumsaidia.

“Kuna kitu watu wala hawakizungumzii, ambacho ni tabia

nzuri ya mtu baada ya beki huyo kumsaidia mchezaji huyo wa Mali uwanjani.”

Baadaye Aurier alisababisha mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya mechi hiyo mjini Bouake, ambayo Ivory Coast walishinda mabao 3-1, baada ya kujikaba shingo akishangilia bao la pili aliloifungia nchi yake.

Mataifa hayo mawili ambayo yanapakana, yamekuwa na uhasimu mkubwa kwenye soka.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, alipamba vichwa vya habari kwa kufungwa kifungo cha nje cha miaka miwili kwa kumpiga polisi kiwiko, ingawa nchini Ufaransa kwa kifungo kifupi kama hicho unaruhusiwa kusafiri.

Msimu uliopita pia aliingia kwenye utata na klabu yake, baada ya kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye mtandao wa kijamii.

Baada ya kuandika ujumbe huo wa kupinga mapenzi ya jinsia moja ‘aliwatagi’ kocha wake wa PSG wakati huo akiwa Laurent Blanc na wachezaji wenzake, akiwemo nyota wa sasa wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic.

Aurier alifungiwa na klabu yake kwa wiki tano kwa kosa hilo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -