Tuesday, November 24, 2020

SERIKALI IMEWANG’ATA SIKIO TFF, KAZI KWENU WAAMUZI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

KUELEKEA pambano la watani wa jadi kwenye soka la Tanzania, Simba na Yanga, Jumamosi hii, Serikali imetoa tahadhari kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha wanapanga waamuzi wazuri wenye maadili ya kutosha.

Rai hiyo imetolewa na Serikali baada ya kurejea mchezo wa Oktoba mosi mwaka jana uliosababisha vurugu na kufanya mashabiki kuharibu miundombinu ya Uwanja wa Taifa kwa kuvunja viti na milango baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo, Martin Saanya.

Vurugu hizo zilitokea baada ya mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, kushika mpira kabla ya kufunga bao la kuongoza na kisha kumpa kadi nyekundu nahodha wa timu hiyo, Jonas Mkude dakika ya 29 jambo lililowakera mashabiki wa Simba waliomaliza hasira zao kwenye kung’oa viti. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1.

Kutokana na vurugu hizo, Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, chini ya Waziri Nape Nauye, iliuzuia uwanja huo pamoja na mapato ya mchezo huo hadi ilipokata gharama za uharibifu uliosababishwa na vurugu hizo ambapo mwishoni mwa mwezi uliopita Serikali ikaziruhusu timu hizo kutumia tena uwanja huo.

Mbali na kufungia uwanja huo, pia Bodi ya Ligi (TPLB) kupitia kamati ya usimamizi na uendeshaji, iliwaondoa kwenye ratiba waamuzi Martin Saanya na mshika kibendera Samweli Mpenzu waliochezesha pambano hilo kutokana na kushindwa kusimamia vyema sheria 17 za mchezo wa soka.

Lakini Jumamosi hii nchi ‘itasimama’ kwa dakika 90 kama kawaida kupisha mechi hii ya watani wa jadi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, kutokana na kugusa hisia za Watanzania wengi ndani na nje ya nchi  kwa sababu za kihistoria.

Bado waamuzi watakaochezesha ‘derby’ hiyo hawajajulikana kutokana na kamati ya waamuzi kutokaa kikao cha kujadili mwamuzi atakayeweza kusimamia sheria 17 za soka siku hiyo.

Yapo makosa yanayofanywa  kibinadamu lakini bado mwamuzi anahitajika kuwa makini na kudhibiti makosa yasijirudie mara kwa mara, kwani yanahatarisha mambo mengi uwanjani.

Waamuzi wengi wanatupiwa lawama kwa kushindwa kutafsiri vema sheria 17 zinazotawala katika mchezo wa soka kwa kuonyesha upungufu mkubwa hasa katika mechi zinazohusisisha timu zenye upinzani mkubwa.

Wapo waamuzi wengi wenye uwezo mkubwa wa kuchezesha michezo, lakini kinachoonekana ni ukiritimba wa viongozi wa shirikisho hilo wa kuwapitisha waamuzi ambao hawakufaulu vizuri mitihani ya waamuzi maarufu kama ‘Cooper test’.

Lakini kama waamuzi wakisimamia sheria 17 za soka basi watakuwa salama na watajiepusha na rungu kama walilolipata wakina Saanya.

Natoa rai kwa waamuzi watakaochezesha mechi hiyo Jumamosi kujua wana jukumu la kutoa maamuzi sahihi.

Ndiyo maana sasa Serikali imeamua kuingilia kati kutoa neno kwa TFF, hivyo jukumu sasa ni kwenu waamuzi kwani nyie mtakaoteuliwa kuchezesha mechi hiyo ndiyo mtakuwa na dhamana kubwa ya kulijenga upya soka la Tanzania hasa katika mechi ya watani ambayo imekuwa haiishi malalamiko hasa kwa waamuzi.

Kila la kheri waamuzi watakaochezesha pambano hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -