Sunday, November 1, 2020

SERIKALI INATAKA NINI SIMBA, YANGA?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

YANGA 1935, Simba 1936. Hiyo ndiyo miaka ambayo klabu hizi kongwe zilianzishwa rasmi na kupata utambulisho wake kutoka Serikali ya wakati huo. Pamoja na mambo mengine klabu ya Yanga ikiitwa Dar es Salaam Young Africans ilikuwa ni klabu ya kimkakati katika mapambano ya kupata uhuru wa nchi yetu.

Simba iliitwa Sunderland na baadaye klabu hizi mbili zilikuwa Simba na Yanga zikiwa ni timu pinzani tangu enzi za kuanzishwa kwao, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika klabu zilizokuwa za kimkakati zilikuwa na upinzani wa hali ya juu.

Leo si lengo langu kueleza historia ya Yanga na Simba, lakini ukiangalia kwa namba utaona kwamba klabu hizo zina umri mkubwa sana, na kama ingekuwa ni umri wa binadamu tunazungumzia mtu mwenye vitukuu sasa, tena vitukuu vyenyewe vipo chuo kikuu.

Kwa Yanga ni miaka 81, ambayo kwa hesabu za miaka 20 kupata mtoto maana yake ni vizazi vinne kwa maana kwamba baba akizaa mtoto akiwa na miaka 20, mwanawe akazaa akiwa na miaka 20, hivyo baba anakuwa na miaka 40 kapata mjukuu, mjukuu akizaa akiwa na miaka 20, babu anakuwa na miaka 60, aliyezaliwa naye akizaa akiwa na miaka 20, huyo kikongwe anakuwa na miaka 80 na hicho kilichozaliwa sasa kina mwaka mmoja.

Ukiziangalia klabu hizi kimaendeleo haziendani na umri wake, zimechoka na zimekuwa ombaomba kwa miaka mingi zikitegemea ufadhili wa watu. Klabu zimekuwa tegemezi licha ya kuwa na mtaji mkubwa wa kuwa na wafuasi wengi ambao kimsingi katika mpira wa miguu ndiyo utajiri wenyewe.

Je, ni sababu gani inazifanya klabu hizi kuendelea kuwa ombaomba? Jibu ni rahisi tu, uendeshaji, zimekuwa klabu za kijamaa tangu enzi za ujamaa hadi leo hii ambapo mambo yameshabadilika kabisa.

Simba na Yanga zilikuwa klabu za ridhaa na hiyo haikuwa na shida kabisa wakati ule wa harakati za Mwalimu Julius K. Nyerere. Zilikutanisha watu wa michezo ya aina mbalimbali ambao walicheza na kupanga mambo yao.

Baada ya Uhuru mwaka 1961 na baadaye kuingia awamu ya pili ya uongozi wa Taifa letu mwaka 1985, klabu hizi zilitakiwa kujibadilisha, si kubadilika kwa maana nyingine lakini mfumo wake ulitakiwa kubadilishwa sanjari na mabadiliko ya katiba za klabu hizo yalivyokuwa yakifanyika.

Kwa bahati mbaya hadi wakati huo bado tulikuwa katika mpira na michezo ya ridhaa, kama taifa linaloendelea pengine bado tulikuwa mbali na mawazo kwamba michezo ni kazi na ni biashara.

Baada ya mabadiliko makubwa katika sekta ya mchezo duniani kote, hatimaye Tanzania ilikubali kuingia kwenye mgumo wa soka la kulipwa takribani miaka 20 iliyopita.

Licha ya kuingia huko bado mfumo wa klabu zetu hizi za Yanga na Simba ni ule ule wa kijamaa ambao hauzipi nafasi ya kusonga mbele kimaendeleo. Klabu zingine zote zinazoendeshwa kwa mfumo wa wanachama kama ilivyo kwa Yang na Simba zimepiga hatua kubwa mno na zingine ndio hizo zinazotawala soka la dunia.

Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich ni timu zenye mafanikio mkubwa sana, hizi ni klabu za wanachama, lakini zilikubali kubadili mifumo ya uendeshaji zikaingia katika biashara bila kuathiri utambulisho wao na leo ndio klabu zenye mafanikio makubwa sana.

Kwa Tanzania Simba na Yanga zimechelewa sana, lakini kwa sasa zinalazimika kwenda katika mfumo mpya, kwanza ili kwenda sanjari na soka la kidunia, lakini pili ni kukabiliana na hali ya utegemezi uliopo anbapo baadhi ya watu wamekuwa wakibeba mzingo mkubwa kuzifadhili klabu hizi ambapo hatari yake watu hawa wakichoka klabu hizi zitashindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake wa kawaida achilia mbali wachezaji.

Klabu hizi zimekuwa na michakato yake ya mabadiliko, lakini michakato hii imekutana na kigingi cha Serikali kupia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambalo sasa kwa mara ya tatu linakuja na tamko ambalo linaashiria kutotaka mabadiliko kwenye klabu hizo kongwe.

Awali BMT kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake, Mohammed Kiganja ilitoa kauli ambayo ilionekana kama ni mwongozo wa klabu hizo kufikia mabadiliko wanayoyahitaji, lakini mwongozo huo uliambatana na maneno mengine mengi ambayo kimsingi tafsiri yake ilikuwa ni kama vile BMT haikubaliani na mabadiliko.

Klabu ziliendelea na.michakato yao kama ilivyokuwa imeelekezwa na zote mbili haikuwa rahisi sana kurudi kuanza upya, zilibadilisha tu mwelekeo kwa kuanza kufuata njia bora iliyoelekezwa na Serikali.

Jambo la ajabu ni kwamba, hata baada ya klabu kupanga kuanza kufuata njia hizo kama kufanya kwanza mabadiliko ya Katiba zao, ili mabadiliko hayo yatokane na katiba hizo bado BMT imeonyesha kutokubali.

Yanga walipoitisha mkutano wao wa dharura, mbali na baadhi ya wanachama kwenda mahakamani kuupinga, lakini BMT ilikuja na kauli ya kusimamisha michakato hiyo kwa klabu zote na kuzitaka zifuate utaratibu katika michakato ya Katiba zao.

Pamoja na maelekezo mazuri ya Serikali kupitia BMT lakini pengine maneno aliyoyasema Kiganja yalikuwa makali zaidi na kuwafanya wadau wengine kujiuliza maswali mengi juu ya mtazamo wa Serikali yetu hii juu ya klabu za Simba na Yanga.

Kiganja alisema Yanga na Simba ni timu za wanachama, hivyo hawezi kupewa mtu binafsi na kama mtu huyo anataka aanzishe timu yake. Maneno haya yalikuwa makali mno ambayo yaliwalenga moja kwa moja watu waliotaka kuwekeza pesa zao kwenye klabu hizi au watu ambao wamekuwa wakitoa pesa zao kisaidia mambo muhimu ya uendeshaji katika klabu hizi.

Kimsingi nilitegemea serikali ingeunga mkono mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Simba na Yanga na ingejenga mazingira mazuri zaidi ya kufanikisha mabadiliko hayo kwa msingi wa kufuata, taratibu, kanuni na sheria za nchi.

Nilidhani kwamba Serikali inakerwa na matokeo mabovu ya timu zetu kwenye ngazi za kimatifa na nilifikiri kwamba Serikali inataka kuona mabadiliko kwenye mchezo wa soka.

Lakini kwa hali inavyoonekana ni kwamba bado Serikali haitaki mabadiliko yatokee kwenye soka. Najiuliza kwanini sasa mvutano umekuwa baina ya Serikali na klabu? Je, Serikali inafaidika nini na klabu za Yanga na Simba katika mfumo huu wa sasa?

Ninaamini klabu hizi zinahitaji mabadiliko makubwa sana ambayo yatazifanya kuinufaisha pia serikali kwa mapato makubwa zaidi lakini pia katika kuleta heshima katika soka la kimataifa. Mafanikio ya soka la kimataifa hayawezi kuja kwa aina hii ya uendeshaji wa klabu zetu.

Nategemea BMT itajitafakari na kujiangalia upya, juu ya uamuzi na kauli zake. Nafahamu sheria ya BMT imepitwa na wakati, sera ya michezo pia imepitwa na wakati. Hivyo jambo la msingi ambalo BMT ilitakiwa kujikita kwa sasa ni kuhakikisha inahusisha sheria na sera ya michezo ili kwenda sambamba na wakati.

Dunia imebadilika na Tanzania ni sehemu ya mabadiliko hayo, hivyo BMT kuendelea kung’ang’ania klabu hizi zijiendeshe kwa mfumo wa ujima ni kuziua. Na nahisi siku si nyingi BMT itakuwa adui mkubwa wa Yanga na Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -