Tuesday, October 20, 2020

‘Serikali tengenezeni ajira, tuachieni Yanga yetu’

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HUSSEIN OMAR

WANACHAMA wa Yanga wameitaka Serikali kutowaingilia katika mikakati yao ya kuifanya klabu hiyo kujiendesha kisasa zaidi na badala yake kuitaka kuumiza vichwa kuona ni vipi inaweza kutatua tatizo sugu la ajira linalowakabili vijana na hata watu wazima kwa sasa.

Tamko hilo limekuja siku chache tangu Serikali kupitia kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohammed Kiganja, kupiga marufuku michakato yote ya mabadiliko ya mifumo inayofanywa na Simba na Yanga ya aidha kukodisha au kuziendesha kwa mfumo wa hisa.

Wakati Yanga ikiwa inajipanga kuikodisha klabu yao kwa Kampuni ya Yanga Yetu kwa mkataba wa miaka 10, Simba wao walikuwa wakijiandaa kuiendesha klabu yao kwa mfumo wa hisa, huku mwanachama wao maarufu, Mohammed Dewji (Mo), akipanga kununua hisa asilimia 51.

Michakato hiyo ilionekana kupokewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa soka hapa nchini, baadhi wakipinga, huku wengine wakisapoti kwa kile walichoamini ndio suluhisho la kuzikwamua klabu hizo kutoka katika ukata unaozikabili na kubaki kuwa omba omba.

Ni kutokana na hayo, mapema wiki hii Serikali iliamua kutoa tamko rasmi kwamba klabu yoyote hairuhusiwi kubadili mfumo wa uanachama kwenda umiliki wa hisa au ukodishwaji hadi pale marekebisho ya katiba zao yatakapofanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za BMT na kanuni za msajili namba 442, kanuni ya 11, kifungu kidogo cha (1-9).

Kiganja alisema mabadiliko hayo yanayoendelea kwenye klabu hizo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya wanachama kwenda mahakamani kupinga michakato hiyo.

Wakijibu tamko hilo la Serikali, wanachama wa Yanga wameliambia BINGWA jana kuwa kwa sasa hawapo tayari kurudishwa nyuma katika mikakati yao ya kujikwamua kiuchumi, lakini pia kuwakatia mirija wale wote ambao wamekuwa wakinufaika binafsi kupitia klabu hiyo, huku wachache wakitoa fedha zao kuigharamia timu, kuanzia usajili wa wachezaji, mishahara yao na ya makocha wao, lakini pia maandalizi ya mechi mbalimbali kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mwanachama maarufu wa Yanga, Edwin Kaisi, alisema ni vyema Serikali ikawaachia timu zao na kuendelea mipango yao, hasa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania, zaidi ikiwa ni umasikini uliopitiliza kuliko kuwaingilia na kuipiga marufuku mipango hiyo.

“Sisi tunasema ya Kaisari mpe Kaisari. Wanatuvuruga tu, hatutaki Serikali iingilie kati kuhusu masuala yetu ya ukodishwaji. Kuna changamoto mbalimbali zinazotukabili vijana wa Tanzania na hata watu wazima ya ukosefu wa ajira, hivyo Serikali iumize vichwa kuona ni vipi inatatua kero hizi badala ya kuzigeukia klabu ambazo kwetu sisi ni kama kimbilio la kujifariji kutokana na ugumu wa maisha unaotukabili kwa sasa,” alisema.

Kaisi alisema wanashangaa kuona Serikali imeonyesha kuguswa mno na michakato inayofanywa na Simba na Yanga, wakati timu hizo zinapokabiliwa na matatizo ya kifedha, hasa mishahara ya wachezaji na mengineyo, haiwasaidii kwa lolote zaidi ya kukimbilia kuwakata kodi ya mapato ya mechi mbalimbali za ligi na michuano mingineyo.

“Serikali lazima ifahamu kuwa klabu za Yanga na Simba ni taasisi kubwa na zenye kuvuta hisia kali kwa mashabiki wake, sasa unapoziingilia, unaweza kusababisha matatizo makubwa…watuachie tu mambo yetu ambayo kimsingi huwa tunakubaliana wenyewe katika vikao vyetu halali,” alisema Kaisi.

Aliongeza kuwa wao kama wanachama wa Yanga waliridhia kwa kauli moja kuikodisha timu yao, lakini wanashangazwa na kitendo cha Serikali kuingilia masuala yao kwa kuwafuata waliowaita watu wachache wanaopinga mabadiliko ambayo wanahofia kupoteza fursa zao za kujinufaisha binafsi kupitia klabu hizo, hasa uuzaji wa jezi na bidhaa mbalimbali kwa kupitia majina ya Simba na Yanga.

“Miaka nenda rudi, timu hizi zimekuwa masikini, leo wanapatikana watu wa kuziendesha, lakini wanakwamishwa na watu wachache wasiotutakia mema, hii si sahihi. Serikali ituachie timu zetu na kuangalia ni vipi inaweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania, zikiwamo uhaba wa dawa hospitalini, chakula, vifaa na huduma kadha wa kadha za shuleni na nyinginezo za kijamii,” alisema.

Tangu klabu za Simba na Yanga zilipoanzishwa takribani miaka 80 iliyopita, zimekuwa zikitegemea hisani za watu wachache kutokana na kukosa vitega uchumi, huku pia viwanja vya mazoezi vikiwa ni shida kwao na matokeo yake kuishia kutangatanga huku na huko.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -