Wednesday, November 25, 2020

SERIKALI YAWAONYA VIONGOZI PST

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA GLORY MLAY

SERIKALI kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limewaonya viongozi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), kuendelea kujihusisha na masuala ya ndondi.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja, alisema Rais wa PST, Emmanuel Mlundwa na katibu wake, Antony Rutha, wanaendelea na majukumu licha ya kufungiwa kwao.

Kiganja alisema viongozi hao wanaendelea kuwaandalia mabondia nchini mapambano nje ya Tanzania kinyume cha sheria.

Alisema wamekuwa wakisafirisha mabondia bila kufuata utaratibu, hivyo anakemea kitendo hicho.

Kiganja alisema ni jambo la hatari kuwapeleka mabondia nje ya nchi bila kufuata sheria, kwani wakipata matatizo watashindwa kuwajibika.

Kauli ya katibu huyo imekuja baada ya bondia Julias Kisarawe kwenda Urusi kukipiga na Apti Usatarkhanov, katika pambano lisilo la ubingwa litakalopigwa leo katika Ukumbi wa Colosseum Sport Hall, mjini Grozny.

Pambano hilo la uzani wa Super Feather litapigwa kwa raundi 10 ambapo bondia Kisarawe aliondoka nchini jana.

Awali Rutha, alisema bondia huyo amefanya mazoezi ya kutosha na ana ari ya ushindi.

Rutha alisema kutokana na maandalizi aliyofanya bondia huyo ana imani kubwa ataipeperusha vema bendera ya Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -