Sunday, January 17, 2021

Serikali yazuia mabadiliko Simba, Yanga

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

SERIKALI kupitia Baraza la Taifa la Michezo (BMT), imepiga marufuku kuendelea kwa michakato yote ya mabadiliko ya mifumo inayofanywa na klabu za Simba na Yanga.

Agizo hilo la Serikali limetolewa jana na Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa timu yoyote hairuhusiwi kubadili mfumo kutoka wanachama kwenda umiliki wa hisa au ukodishwaji hadi pale marekebisho ya katiba zao yatakapofanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za BMT na kanuni  za msajili namba 442 kanuni ya 11 kifungu kidogo cha (1-9) yatakapofanyika.

Kiganja alisema mabadiliko hayo yanayoendelea kwenye klabu hizo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya wanachama kwenda mahakamani kupinga michakato hiyo, lakini pia kupeleka malalamiko Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na BMT kitu ambacho si ishara nzuri endapo yataachwa yaendelee.

“Tumesitisha michakato yote ya kubadili umiliki kutoka kwa wanachama kwenda kwa uwekezaji kwa timu za Simba na Yanga mpaka watakapofanya mabadiliko kwa mujibu wa katiba za klabu zao kwa kufuata sheria zilizowekwa.

“Iwapo kama timu moja kati ya hizi zitaamua kukiuka agizo hili kwa kuendelea na mchakato huu kabla ya taratibu za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.

Alisema iwapo kama kuna mdau au mwanachama yeyote anayetaka kufanya uwekezaji kwenye klabu zinazomilikiwa na wanachama ni vema angeanzisha timu yake kama Saidi Bakhresa alivyoanzisha Azam FC ili kupunguza malalamiko.

Kiganja alisema kilichofanywa na klabu za Simba na Yanga ni makosa kikatiba kwani michakato hiyo ilitakiwa ianzie kwenye matawi nchi nzima ili maamuzi yawe ya wote na kama ilivyokuwa ambapo inaonekana maamuzi mengi yanayotolewa yanawashirikisha wachache.

Kiganja alisema tayari wameshapeleka barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kuzuia jambo hilo ili waweze kuwapa taarifa wanachama wao na wana hakika hakuna atakayefanya jambo kinyume na maamuzi ya Serikali inayoongozwa kwa kutumia katiba.

Kuali hiyo ya Serikali imekuja miezi michache tu tangu klabu ya Simba kutaka kuingia katika mfumo wa hisa kwa kumkabidhi timu mfanyabiashara mkubwa Afrika, Mohamed Dewji (Mo) ambaye anataka asilimia 51 huku wanachama wakibaki na 49.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Wanamsimbazi, Jangwani nako kupitia mkutano wao mkuu uliofanyika Agosti 6 mwaka huu, waliridhia ombi la Mwenyekiti wao kuikodisha Yanga kwa miaka 10 kwa kuchukua timu na nembo huku kila mwaka akiwapa asilimia 25 ya faida na yeye kubaki na 75.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -